-
Kongamano la Kimataifa la Kiswahili lafanyika Zanzibar+SAUTI
Dec 13, 2018 12:28Zanzibar ni mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Kiswahili. Kongamano hilo la siku mbili limefunguliwa rasmi na Rais Dkt Ali Mohammad Shein, ambaye amesisitiza haja ya kuenziwa magwiji na waandishi wa vitabu vya Kiswahili. Mwandishi wetu wa Zanzibar Harith Subeit ana maelezo zaidi......
-
Rais Uhuru Kenyatta aongoza Wakenya katika maadhimisho ya Jamhuri Day + Sauti
Dec 12, 2018 13:27Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Jumatano ya leo amewaongoza Wakenya kuadhimisha miaka 55 ya uhuru wa nchi hiyo (Jamhuri Day) huku maelfu ya raia wakijitokeza katika viwanja mbalimbali nchini humo kuadhimisha siku hii. Saifullah Murtadha mwandishi wetu wa Mombasa ametuandalia ripoti ifuatayo.
-
Wanasiasa wa upinzani Uganda wakutana mjini Kampala + Sauti
Dec 12, 2018 13:22Wanasiasa wa vyama kadhaa nchini Uganda wamekutana katika mji mkuu wa nchi hiyo Kampala katika mjadala maalumu uliogusia masuala muhimu kadhaa ya kijamii na kisiasa kuhusu mustakbali wa nchi hiyo. Kigozi Ismail mwandishi wetu wa Kampala ametuandalia taarifa ifuatayo.
-
Uganda nayo yaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu + Sauti
Dec 10, 2018 14:43Uganda imejiunga na nchi nyingine dunia katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Haki za binadamu. Sherehe hiyo imehutubiwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye ametangaza mkakati mpya wa kupambana na ufisadi ambao umeutaja kuwa ni sawa na maradhi ya saratani. Kigozi Ismail na ripoti kamili...
-
Kenya yaorodheshwa kati ya nchi zisizochunga haki za binadamu kwa raia + Sauti
Dec 10, 2018 14:37Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeiorodhesha Kenya miongoni mwa mataifa ambayo hayajazingatia kikamilifu haki za raia wake duniani. Ripoti ya shirika hilo iliyozinduliwa leo Jumatatu imeiorodhesha Idara ya Polisi ya Kenya kuwa inaongoza katika ukiukaji wa haki hizo. Mwandishi wetu wa Kenya, Seifullah Murtadhaa anayo maelezo zaidi...
-
Viongozi wa Waislamu Zanzibar wataka kufungwa mabaa visiwani humo
Dec 09, 2018 04:11Viongozi wa Kiislamu Zanzibar nchini Tanzania wameitaka serikali ifunge mabaa na vituo vya vileo wakisisitiza kuwa vinachangia katika mmomonyoko wa maadili katika visiwa hivyo.
-
Rais wa Kenya atetea kumteua Moody Awori kuongoza bodi ya hazina ya vijana + Sauti
Dec 08, 2018 14:23Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ametetea uamuzi wake wa kumteua Makamu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Moody Awori mwenye umri wa miaka 91 kuongoza bodi ya hazina ya vijana. Maelezo zaidi yamo kwenye ripoti ya mwandishi wetu wa Kenya, Seifullah Murtadha.
-
33 Wajeruhiwa katika maandamano ya 38 ya Haki za Kurejea Palestina + Video
Dec 08, 2018 12:06Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza leo kuwa, Wapalestina 33 wamejeruhiwa katika maandamano ya jana ya Ijumaa ya 38 ya Haki ya Kurejea yaliyofanyika kwenye mpaka wa Ukanda wa Ghaza na ardhi nyingine za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
-
Shirika la mafuta na gesi la Uganda latambuliwa rasmi kimataifa + Sauti
Dec 03, 2018 23:35Shirika la kwanza la mafuta na gesi la Kigumba, magharibi mwa la Uganda latambuliwa rasmi kimataifa. Mwandishi wetu Kigozi Ismail na maelezo zaidi
-
Tume mpya ya ukweli na maridhiano Burundi yaanza kazi + Sauti
Dec 03, 2018 23:32Mwenyekiti mpya wa tume ya ukweli na maridhiano ya nchini Burundi amekula kiapo mbele ya Rais Piere Nkurunziza wa nchi hiyo. Maelezo zaidi yamo kwenye ripoti ya mwandishi wetu, Hamida Issa...