Hamas: Idi ya kweli ya Wapalestina ni kukombolewa Quds tukufu
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, amesema kuwa harakati hiyo itadumisha mapambano yake dhidi ya utawala ghasibu wa Israel hadi Palestina itakapokombolewa.
Abu Ubaida mbaye ni msemaji wa tawi la kijeshi la Hamas amesema idi ya kweli na halisi ya watu wa Palestina itatimia pale Palestina na Msikiti mtakatifu wa al Aqsa utakapokombolewa kutoka kwenye makucha ya Wazayuni maghasibu.
Abu Ubaida amesema mazungumzo ya aina yoyote na Wazayuni hayana faida kwa taifa la Palestina na kwamba utawala wa Israel haujiu isipokuwa vita.
Wakati huo huo harakati ya Jihad Islami ya Palestina imewataka viongozi wa nchi za Waislamu na Kiarabu kufanya jitihada za kukomboa eneo alikotokea Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad (saw) kuelekea mbinguni huko Baitul Muqaddas.