Muqawama wa Iraq wapiga kambi ya kijeshi ya Marekani huko Syria
(last modified Thu, 18 Jan 2024 11:48:53 GMT )
Jan 18, 2024 11:48 UTC
  • Muqawama wa Iraq wapiga kambi ya kijeshi ya Marekani huko Syria

Televisheni ya al Mayadeen imetangaza kuwa wanamuqawama wa Iraq wameishambulia kambi ya kijeshi ya Marekani ya hemo huko Syria kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

hemobase n syraWakati huo huo vyanzo vya ndani vimeripoti kutekelezwa mashambulizi dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani huko Syria, sambamba na kuendelea chokochoko za Marekani na Uingereza huko Yemen. 

Televisheni ya al Mayadeen imetangaza kuwa wanamuqawama wa Kiislamu wa Iraq wametumia ndege zisizo na (rubani droni) kuipiga kambi ya kijeshi ya wanajeshi vamizi wa Marekani ya Hemo huko Syria. 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kituo hicho cha kijasusi cha Marekani kiko magharibi mwa uwanja wa ndege wa Qamishli na mamluki wa utawala wa Kizayuni pia walikuwepo ndani ya kituo hicho. 

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Iraq cha "Sabrin News", hili ni shambulio la pili kutekelezwa dhidi ya kambi ya Hemo tangu utawala haramu wa Kizyauni uanzishe vita dhidi ya  Gaza. 

Muqawama wa Iraq hadi sasa umeshambulia kwa mara kadhaa kambi za ujasusi za Marekani huko mashariki na kaskazini mashariki mwa Syria, na pia huko magharibi na kaskazini mwa Iraq kwa kutumia droni na maroketi. 

Kambi ya ujasusi ya Marekani ya Hemo huko Syria yashambuliwa kwa droni na muqawama wa Iraq 

Muqawama wa Iraq unaitambua Marekani kuwa mhusika mkuu wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni  ukanda wa Gaza na unasisitiza kuwa, utaendeleza  mashambulizi dhidi ya Marekani hadi hapo hujuma za kikatili dhidi ya Gaza zitakapositishwa.