Mkutano wa mawaziri wa Kiarabu Riyadh wataka kuhitimishwa vita vya Gaza
Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa mataifa matano ya Kiarabu walmekutana Riyadh mji mkuu wa Saudi Arabia na kuutoa mwito wa kusitishwa vita huko Gaza.
Katika kikao chao kilichofanyika mjini Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, mawaziri hao wamesisitiza juu ya ulazima wa kuhitimishwa vita vya Ukanda wa Gaza na kufikiwa makubaliiano ya kumalizwa vita hivyo.
Katika mkutano wao huo wa mashauriano, Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Saudi Arabia, Qatar, Imarat, Misri na Jordan sambamba na Hussein al-Sheikh, Kkatibuu wa Kamatii ya Utendajii ya Harakati ya Ukombozi wa Palestina PLO wamesema kuuwa, kuna haja ya vita vya Gaza kkuhitimishwa kkwani hali ya kibinadamu katikak Ukanda huo ni mbaya.
Aidha washiriki wa mkutano huo wametangaza himaya yao kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).
Siku chache zilizopita maripota wa Umoja wa Mataifa walitangaza kwamba wanalaani vikali jaribio lolote la kuchafua sura ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA).

Baadhi ya nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zimekata misaada yao kwa shirika hilo la Umoja wa Mataifa kutokana na madai yasiyo na msingi yaliyotolewa na utawala katili wa Israel. Awali, Yisrael Katz Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Israel alitoa mwito wa kujiuzulu Philippe Lazzarini, Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) akikariri tuhuma kwamba wafanyakazi kadhaa wa UNRWA walishiriki katika shambulio la wapigania uhuru wa Palestina dhidi ya Israel, tarehe 7 Oktoba.
Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa Israel naye amewahi kudai kuwa, umewadia wakati sasa shirika la UNRWA lihitimishe shughuli zake huko Gaza.