Kufanyika kura ya maoni Palestina; mkakati na suluhisho la Iran
Nasser Kanani, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amesema kuwa, "suluhisho bora zaidi la kuhitimisha hali haramu ya sasa katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu ni kufanyika kura ya maoni jumuishi kwa kushirikisha wakaazi wote na raia asili wa ardhi hiyo."
Mahakama ya Kimataifa ya Haki siku ya Ijumaa iliashiria ujenzi na upanuzi wa vitongoji vya walowezi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Quds Mashariki na kutaja uwepo wa utawala wa Kizayuni katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu kuwa ni kinyume cha sheria na kutaka kukomeshwa hatua hizo.
Tangu tarehe 7 Oktoba 2023 utawala unaofanya mauaji ya kimbari wa Israel kwa uungaji mkono kamili wa nchi za Magharibi hususan Marekani umefanya mauaji makubwa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya watu wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina. Kimya cha jamii ya kimataifa na taasisi za kutetea haki za binadamu kuhusiana na jinai za utawala unaoikalia kwa mabavu Palestina kimesababisha kuendelea kuuawa wanawake na watoto wa Kipalestina na jeshi la utawala haramu wa Kizayuni. Tangu Oktoba 7, 2023, takriban Wapalestina 39,000 wameuawa shahidi na takriban 90,000 wamejeruhiwa.
Licha ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kupasisha uamuzi wa kukomeshwa uvamizi wa Palestina na hata kulitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuchukua jukumu la utekelezaji wa uamuzi huu, lakini hadi sasa hakuna mpango wa dhati wa kumaliza uvamizi huo uliopendekezwa na kuchungwa haki ya wananchi wa Palestina ya kujiainishia hatia yao.
Moja ya mipango mizito iliyowasilishwa kuhusiana na suala hili ni kutoka kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inasisitiza ulazima wa kufanyika kura ya maoni baina ya Wapalestina ili kubainisha hatima ya ardhi hiyo. Mtazamo huu haukuishia kwenye hotuba ya Kiongozi wa Muadhamu au kubakia kama wazo tu, na uliwasilishwa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika fremu ya mpango wa kidiplomasia kwa Umoja wa Mataifa na kusajiliwa katika umoja huo.
Kwa mujibu wa mpango huo, suluhisho pekee ni kuitisha kura ya maoni ya kitaifa kwa kushirikisha Wapalestina wote wakiwemo Waislamu, Wakristo, Wayahudi na watoto wao. Mbali na kuwa wa kidhalimu, kikoloni na usio wa kibinadamu mpango wa kuifanya Palestina kuwa ya Kizayuni, sisitizo la wananchi wa Palestina la kutaka kufanyika kura ya maoni linapata umuhimu maradufu kwani nchi za Magharibi katika miaka yote ya baada ya kuundwa utawala bandia wa Kizayuni hazijajaribu kutatua suala la Palestina kupitia maoni ya wakaazi wa eneo hilo.
Hii ni pamoja na kwamba, kufanyika kura za maoni, uchaguzi, kuegemea maoni na demokrasia ya watu kumekuwa suluhisho kuu na sisitizo la Iran kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Palestina katika miaka yote hii, suluhisho ambalo ukoloni, Magharibi, Uingereza na Marekani zimekuwa zikilikwepa tangu miaka mia moja iliyopita.
Kuhusiana na hilo, Nasser Kan'ani, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran akitolea mfano uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki kuhusiana na hatua za utawala wa Kizayuni zinazokiuka sheria za kimataifa ikiwa ni pamoja na kukutaja kukaliwa kwa mabavu na vitongoji vya walowezi wa Palestina katika ardhi hiyo kuwa ni kinyume cha sheria amesisitiza ulazima wa kutolewa fidia kwa uharibifu uliosababishwa kwa Wapalestina.
Nasser Kan'ani amegusia jinsi utawala wa Kizayuni unavyoendelea kupora ardhi za wananchi wa Palestina na kujenga vitongoji haramu vya Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na hukumu ya majuzi ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) na kusema kuwa, kutolewa hukumu hiyo dhidi ya Israel ni uthibitisho wa jinsi dunia nzima inavyoguswa na kadhia ya Palestina.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Mauaji ya kimbari, jinai dhidi ya binadamu na jinai za kivita zinazofanywa na utawala wa Kizayuni hususan huko Gaza ni mambo ambayo yameamsha hisia za walimwengu kutokana na kuona Israel inaendelea kukanyaga haki za wananchi wa Palestina na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa dhidi ya utawala wa Kizayuni.
Kwa mujibu wa mpango huu, suluhu pekee ni kuitisha kura ya maoni ya kitaifa kwa kushirikisha Wapalestina wote wakiwemo Waislamu, Wakristo, Wayahudi na watoto wao.
Mbali na ukatili, ukoloni na unyama wa mpango huo wa kuiwekea Palestina, sisitizo na la kutaka kura ya maoni ya wananchi wa Palestina ni muhimu na maradufu kwani nchi za Magharibi katika miaka yote ya baada ya kuundwa utawala bandia wa Kizayuni hazikuwahi kujaribu kubainisha na kutatua suala la Palestina kwa maoni ya wakaazi wa eneo hilo.
Hii ni pamoja na kuwa, kufanyika kura za maoni, uchaguzi kwa kuegemea maoni na demokrasia ya watu kumekuwa suluhisho kuu na kusisitizwa la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kutatua mgogoro wa Palestina katika miaka yote hii, suluhu ambayo ukoloni, Magharibi, Uingereza na Marekani ilikuwa ikifuata tangu wakati miaka mia moja iliyopita.
Kuhusiana na suala hilo, Nasser Kan’ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran akitolea mfano rai ya Mahakama ya Kimataifa ya Uadilifu (ICJ) kuhusiana na hatua za utawala wa Kizayuni zinazokiuka sheria za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuitaja kukaliwa kwa mabavu Palestina na utawala huo wa Israel na walozezi kujenga vitongoji vyao katika ardhi za Wapalestina katika ardhi hiyo kuwa ni kinyume cha sheria na pamoja na ukiukwaji wa haki ya taifa la Palestina kutumia mamlaka juu ya maliasili Kwa kawaida, alisisitiza ulazima wa fidia kwa uharibifu uliosababishwa kwa Wapalestina.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alisema kuwa; akigusia kutambuliwa kwa mamia ya maazimio na nyaraka za kimataifa kuhusu uhalali wa taifa madhulumu la Palestina.
Amesema kinachotarajiwa kutoka kwa jamii ya kimataifa likiwemo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ni kuchukua hatua za kivitendo za kuiadhibu Israel kwa jinai zake na kulisaidia taifa linalodhulumiwa la Palestina liweze kupata haki lilizoporwa kwa makumi ya miaka sasa.