Russia yawaambia Wazayuni: Hakuna haja ya kuendelea vita Asia Magharibi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i114474-russia_yawaambia_wazayuni_hakuna_haja_ya_kuendelea_vita_asia_magharibi
Msemaji wa Ikulu ya Russia amemshambulia vikali waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, na kusema kuwa, Moscow iko huru katika maamuzi yake na haichukui amri kutoka kwa Wazayuni na inaamini hakuna haja ya kuendelea vita katika eneo la Asia Magharibi.
(last modified 2024-07-25T23:45:36+00:00 )
Jul 25, 2024 23:45 UTC
  • Russia yawaambia Wazayuni: Hakuna haja ya kuendelea vita Asia Magharibi

Msemaji wa Ikulu ya Russia amemshambulia vikali waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni, Benjamin Netanyahu, na kusema kuwa, Moscow iko huru katika maamuzi yake na haichukui amri kutoka kwa Wazayuni na inaamini hakuna haja ya kuendelea vita katika eneo la Asia Magharibi.

Katika hotuba yake ya usiku wa kuamkia jana Alkhamisi, Netanyahu aliishambulia Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa maneno makali katika Baraza la Congress la Marekani na kutaka kuundwe muungano wa kukabiliana na Tehran. 

Akizungumzia pia Russia, Netanyahu alitaka kuundwe muungano kama wa NATO katika eneo la Asia Magharibi lakini mwito huo umepingwa na Msemaji wa Ikulu ya Russia ambaye amesisitiza kuwa, ni jambo lililo mbali kudhani kuwa hali iliyopo hivi sasa inahitaji kutumiwa njia ya vita na makabiliano ya silaha. 

Wazayuni wanatafuta wahalifu zaidi wa kwenda kuingia nao motoni kwa jina zao kama hizi, lakini Russia imekataa

 

Nduli wa Ghaza, Benjamin Netanyahu amepewa jukwaa la kuhutubia ndani ya Baraza la Congress la Marekani katika hali ambayo maelfu ya wananchi wa nchi hiyo walikuwa wamekusanyika nje ya majengo ya baraza hilo kumlaani Netanyahu kwa jinai zake za kutisha dhidi ya wananchi wasio na hatia wa Ukanda wa Ghaza.

Sambamba na kulaani jinai za kutisha za Netanyahu na kundi lake la Wazayuni wenye misimamo mikali na uungaji mkono wa pande zote wa Marekani kwa Israel inayofanya ukatili wa kutisha huko Palestina, waandamanaji hao wamesikika wakitangaza kwa sauti kubwa uungaji mkono wao kwa taifa linalodhulumiwa kila upande la Palestina.

Makumi ya wabunge wa Marekani nao walisusia kikao cha Baraza la Congress ambacho ndani yake Netanyahu alihutubia.