Hizbullah yashambulia maeneo kadhaa Israel kwa droni na makombora
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imeanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya maeneo ya kijeshi ya utawala ghasibu wa Israel, huku kukiwa na hujuma na mashambulio ya Israel kusini mwa Lebanon na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya Wapalestina huko Gaza.
Katika taarifa tofauti iliyotangazwa leo, Hizbullah imeeleza kuuwa, imelenga kwa makombora ya kuongozwa mfumo wa kiufundi katika eneo la Ramia na kupata shabaha moja kwa moja, ambayo imesababisha uharibifu.
Aidha harakati hiyo ya muqawama iimesema, Kundi hilo la upinzani pia lilisema kuwa wapiganaji wake wamelenga mkusanyiko wa wanajeshi wavamizi wa Israel ndani ya eneo la Hadab Yaron.
Vyombo vya habari vya Lebanon vikiriipoti kutoka kusini mwa Lebanon vimethibitisha kuwa, yameonekana makombora yaliyokuwa yakirushwa moja kwa moja uligunduliwa kutoka Lebanon na kulenga maeneo ya kijeshi yaa Israel katika maeneo ya Ramia na Hadab Yaron.
Hivi karibuni Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon alitoa onyo kwa Wazayuni wakati alipohutubia marasimu ya Ashura huko Beirut kwamba: Muqawama wa nchi yake utavishambulia vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni ambavyo hadi sasa havijalengwa na mashambulizi.
Tangu kuanza operesheni za Hizbullah huko kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel); walowezi wengi wa Kizayuni katika eneo hilo wamelazimika kuyahama makazi yao, na kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Kizayuni, aghlabu ya wakazi waliosalia katika eneo hilo wanasumbuliwa na matatizo ya kiakili na kisaikolojia.