Wazayuni: Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel ni "gaidi"
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i115438-wazayuni_waziri_wa_usalama_wa_ndani_wa_israel_ni_gaidi
Idadi kubwa ya walowezi wa Kizayuni wamemshambulia Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakimwita "mharibifu na gaidi".
(last modified 2024-08-20T08:27:38+00:00 )
Aug 20, 2024 08:27 UTC
  • Wazayuni: Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel ni

Idadi kubwa ya walowezi wa Kizayuni wamemshambulia Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni wa Israel wakimwita "mharibifu na gaidi".

Waandamanaji hao wa Israel wamefunga njia mbele ya msafara wa Waziri wa Usalama wa Ndani, Itamar Ben-Gvir, baada ya kupata taarifa ya kuwepo kwake katika kituo cha mafuta katika mji wa Kahal kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Waandamanaji hao wamemtaja Ben Gvir kuwa ni gaidi aliyehukumiwa mahakamani na mharibifu ambaye anaielekeza Israel katika maangamizi. Wamesema Ben Gvir anahitaji matibabu ya kinafsi kisaikolojia.

Waandamanaji hao wamemtuhumu Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel kuwa amepuuza hatima ya mateka wa Israel wanaoshikiliwa katika Ukanda wa Gaza.

Itakumbukwa pia kwamba, familia za mateka hao zilifanya maandamano jana Jumatatu mbele ya makazi alikofikia Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Anthony Blinken, mjini Tel Aviv wakisema Marekani inashirikiana na serikali yenye misimamo mikali ya Netanyahu katika kukwamisha usitisha vita na kuachiwa mateka wa vita huko Gaza.