Muqawama Iraq kuanzisha tena operesheni dhidi ya majeshi ya US
(last modified 2024-08-26T12:19:45+00:00 )
Aug 26, 2024 12:19 UTC
  • Muqawama Iraq kuanzisha tena operesheni dhidi ya majeshi ya US

Makundi ya Muqawama ya kupambana na ugaidi ya Iraq yameafikiana kuanzisha tena operesheni dhidi ya kambi na vituo vya kijeshi vya Marekani katika nchi hiyo ya Kiarabu.

Gazeti la al-Akhbar la Lebanon limenukuu chanzo ambacho hakikutaja jina katika Kamati ya Kuratibu Mapambano ya Iraq (IRCC) kikisema kwamba, wawakilishi kutoka makundi ya Muqawama ya Iraq hivi karibuni wamefanya mkutano na kuamua kuchukua msimamo mmoja kuhusu matukio ya sasa ya ndani na kikanda.

Chanzo hicho kimeongeza kuwa, wengi wa viongozi wa makundi hayo walikubali kusitisha mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Marekani na kuanza tena mashambulizi yao.

Amesema, "Katika mkutano huo, baadhi ya viongozi walizungumzia suala la hatua za kimedani dhidi ya wavamizi wa Marekani na kukubaliana juu ya kuanzishwa tena kwa mashambulizi makubwa dhidi ya majeshi ya Marekani au utawala wa Kizayuni." 

Chanzo kimoja kilichokuwa karibu na mkutano huo kimeripoti kuwa: Kambi ya Muqawama haitatulia madhali majeshi ya kigeni yanaendelea kushambulia Vikosi vya Kujitolea Wananchi vinavyojulikana zaidi kama Hashd al-Sha'abi, na vikundi vingine vya Iraqi.

Kimeeleza kuwa, Muqawama utaendelea na operesheni zake maadamu Marekani inaendelea kuunga mkono na kuupa himaya utawala haramu wa Israel. Wakati huo huo, Harakati ya Asa'ib Ahl al-Haq ya nchini Iraq ameuonya vikali utawala haramu wa Israel dhidi ya kuingia kwenye vita kamili na Harakati ya Hizbullah ya Lebanon.

Tags