Yemen wafanya maandamano ya mamilioni ya watu kuwaunga mkono Wapalestina
(last modified Sat, 31 Aug 2024 04:15:39 GMT )
Aug 31, 2024 04:15 UTC
  • Yemen wafanya maandamano ya mamilioni ya watu kuwaunga mkono Wapalestina

Kwa mara nyingine tena mamilioni ya wananchi wa Yemen wamemiminika barabarani kulaani jinai za utawala wa Kizayuni na kuwaunga mkono wananchi wa Palestina hasa wa Ukanda wa Ghaza.

Jana Ijumaa, zaidi ya maeneo 330 ya Yemen ikiwa ni pamoja na mjini San'a kumefanyika maandamano makubwa ya wananchi Waislamu na wanamuqawama wa Yemen katika kuliunga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina hasa Ukanda wa Ghaza.

Mbali na San'a mikoa mingine kulikofanyika maandamano makubwa ya wananchi wa Yemen ni pamoja na Sa'ada, Ma'rib na mikoa mengine kama ya Umran, Aab, Taiz, Dhamar, n.k.

Kabla ya hapo, Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen alikuwa amesema kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel umevuka mistari yote myekundu, ada na sheria zote za kimataifa.

Sayyid Abdul Malik al-Houthi amesema, jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni ni mauaji ya kimbari na ni doa baya kwa jamii ya binadamu na kuongeza kuwa, amani haiwezi kupatikana kwa njia yoyote maadamu Israel inaendelea  kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Kiongozi huyo wa Ansarullah ya Yemen amesema, katika hali ambayo mgogoro wa Ukanda wa Ghaza unaendelea baada ya takriban mwaka mmoja wa mashambulizi ya kinyama ya utawala ghasibu wa Israel, utawala huo katili hivi sasa umepanua eneo la unyama wake kwa kuvamia na kushambulia maeneo ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan hasa kambi ya Jenin ya wakimbizi wa Kipalestina.