Bahrain yazuia Swala ya Ijumaa na kukamata watu 50 Diraz
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i11782-bahrain_yazuia_swala_ya_ijumaa_na_kukamata_watu_50_diraz
Katika muendelezo wa wimbi la ukandamizaji na dhulma za utawala wa kifalme wa Aal-Khalifa, maafisa usalama nchini Bahrain walizuia Swala ya Ijumaa hapo jana sambamba na kuwatia mbaroni watu 50 katika kijiji cha Diraz, kaskazini magharibi mwa nchi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 22, 2016 23:37 UTC
  • Bahrain yazuia Swala ya Ijumaa na kukamata watu 50 Diraz

Katika muendelezo wa wimbi la ukandamizaji na dhulma za utawala wa kifalme wa Aal-Khalifa, maafisa usalama nchini Bahrain walizuia Swala ya Ijumaa hapo jana sambamba na kuwatia mbaroni watu 50 katika kijiji cha Diraz, kaskazini magharibi mwa nchi.

Polisi walimzuia msomi mashuhuri wa nchi hiyo Sheikh Mohammad al-Sanqour kuongoza Swala ya Ijumaa katika msikiti wa Imam Sadiq katika kijiji cha Diraz na kusababisha hali ya mchafukoge. Waumini waliokuwa wamejitokeza kushiriki ibada hiyo hapo jana walighadhabishwa na hatua hiyo na kufanya maandamano nje ya msikiti huo wakiilaani serikali ya Manama kwa ukandamizaji na kuhujumu uhuru wa kuabudu.

wananchi wa Bahrain wakifanya mudhahara

Waandamanaji hao walikuwa wamebeba mabango yenye picha za mwanachuoni mashuhuri wa Kishia nchini humo Sheikh Isa Qassim.

Ayatullah Sheikh Isa Qassim, mwanachuoni mashuhuri Bahrain aliyevuliwa uraia

 

Wananchi wa Bahrain wamekuwa wakifanya maandamano ya kupinga kuvuliwa uraia Sheikh Isa Qassim kwa tuhuma zisizo na msingi kuwa eti anachochea malumbano ya kimadhehebu na ghasia. Sheikh Qassim ni mashuhuri kwa misimamo yake ya kutetea Umoja wa Kiislamu na maandamano ya amani Bahrain.