Kwa mara nyingine, Israel yashindwa kutungua kombora la Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121048-kwa_mara_nyingine_israel_yashindwa_kutungua_kombora_la_yemen
Mapema leo Jumapili, harakati ya Ansarullah ya Yemen imetangaza kuwa, kombora lililorushwa kutoka nchini humo limepiga kiustadi mkubwa shabaha iliyokusudiwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kwamba madai ya Israel ya kutungua kombora hilo hayana ukweli wowote.
(last modified 2025-01-05T07:58:23+00:00 )
Jan 05, 2025 07:58 UTC
  • Kwa mara nyingine, Israel yashindwa kutungua kombora la Yemen

Mapema leo Jumapili, harakati ya Ansarullah ya Yemen imetangaza kuwa, kombora lililorushwa kutoka nchini humo limepiga kiustadi mkubwa shabaha iliyokusudiwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni na kwamba madai ya Israel ya kutungua kombora hilo hayana ukweli wowote.

Naibu wa Mkuu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kuwa, madai ya utawala wa Kizayuni kwamba umetungua kombora la Yemen nje ya anga ya Israel hayana ukweli wowote kwani ushahidi mbalimbali unathibitisha kuwa, kombora hilo limepiga kwa ustadi wa hali ya juu shabaha iliyokusudiwa. 

Mapema leo asubuhi, Msemaji wa Jeshi la Yemen, Brigedia Jenerali Yahya Saree ametangaza kwamba jeshi la nchi hiyo limeshambulia kituo cha umeme cha Orot Rabin huko Hadera kwa kutumia kombora la balestiki la haypersonic la Palestina-2 na kupiga shabaha wa umakini mkubwa.

Kwa upande wake Kanali ya 12 ya Televisheni ya Israel nayo imethibitisha habari ya kufanyika shambulio hilo.

Kituo cha umeme cha Orot Rabin cha Israel

 

Duru za ndani ya Israel nazo zimesisitiza kuwa, ving'ora vya hatari  vimesikika kila mahali ikiwemo Tel Aviv, mji mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Vyombo vingine vya habari vya Israel vimetangaza kuwa, kumesikika miripuko ya mfululizo katikati ya ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni ambazo zimepachikwa jina bandia la Israel.

Tangu mwaka jana, Jeshi la Yemen limekuwa likiendesha operesheni mbalimbali za kuwaunga mkono ndugu zao Wapalestina hasa wa Ukanda wa Ghaza, ikiwa ni pamoja na kuifunga kabisa Bahari Nyekundu ili vyombo vyote vya Israel na vinavyopeleka mizigo kwa utawala huo katili visiweze kabisa kutumia bahari hiyo na hasa Lango Bahari la Bab al Mandab, hatua ambazo zinaendelea kuisababishia hasara kubwa Israel.