Kukosolewa mauaji ya umati ya Israel katika Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121052-kukosolewa_mauaji_ya_umati_ya_israel_katika_ukanda_wa_gaza
Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichoitishwa kwa ajili ya kuchunguza hali ya Gaza kilifanyika kwa mara nyingine tena. Ukitoa Marekani, washiriki wengine wa mkutano huo wamekosoa "mauaji ya kimbari" ya Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza.
(last modified 2025-01-05T09:01:53+00:00 )
Jan 05, 2025 09:01 UTC
  • Kukosolewa mauaji ya umati ya Israel katika Ukanda wa Gaza

Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kilichoitishwa kwa ajili ya kuchunguza hali ya Gaza kilifanyika kwa mara nyingine tena. Ukitoa Marekani, washiriki wengine wa mkutano huo wamekosoa "mauaji ya kimbari" ya Wazayuni dhidi ya watu wa Gaza.

Katika mwezi wa 15 wa mauaji ya halaiki ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine lilikutana na kutathmini hali ya Gaza.

Suala la kwanza ni kwamba mkutano huu ulifanyika katika hali ambayo huu ulikuwa mkutano wa kwanza wa Baraza la Usalama kuhusu Gaza mnamo 2025.

Mkutano huu pia umefanyika katika hali ambayo, wananchi wa Gaza wanashuhudia mwendelezo wa mashambulizi ya mabomu na mauaji ya Wazayuni mwanzoni mwa mwaka huu mpya. Kuhusiana na hili, Volker Turk, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, ambaye alishiriki mkutano wa Baraza la Usalama kwa njia ya mawasiliano ya Intaneti, alitangaza kwamba "janga la haki za binadamu linaendelea huko Gaza mbele ya macho ya ulimwengu."

Suala jingine ni kwamba kikao cha Baraza la Usalama kilifanyika katika hali ya suutahafamu na utata kuhusu mazungumzo ya kusitisha mapigano. Doha, mji mkuu wa Qatar kwa mara nyingine tena uliandaa mazungumzo ya kusitisha mapigano huko Gaza, lakini bado hakuna dalili za makubaliano kufikiwa huku baraza la mawaziri la Netanyahu likiendelea kuzuia mpango huo.

Karibu Wapalestina 46,000 wameuawa shahidi tangu kuanza mauaji ya kimbari ya Israel katika Ukanda wa Gaza

 

Suala jengine ni kuwa pamoja na kwamba, Baraza la Usalama limeshindwa kupata suluhisho la kusimamisha mauaji ya kimbari ya Wazayuni, na hivyo kuufanya utawala wa Kizayuni uendeleze siasa za mauaji ya kimbari.

Ammar bin Jam’i, mwakilishi wa Algeria amesema katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na suala hilo: Lengo la uvamizi wa Israel huko Gaza ni kuwatimua Wapalestina katika ardhi yao kwa kutumia siasa za mauaji ya kizazi.

Nukta nyingine muhimu ni kwamba, kikao hiki cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kimefanyika baada ya kushambuliwa hospitali ya Kamal Adwan wiki iliyopita na kukamatwa na kuwekwa kizuizini Hussam Abu Safiya, Mkurugenzi wa hospitali hiyo, kitendo ambacho nacho kimelaaniwa katika mkutano huo.

Mwakilishi wa Algeria Ammar bin Jam’i, ambaye ni mwenyekiti  wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alidokeza kuwa, asilimia 63 ya hospitali za Ukanda wa Gaza hazifanyi kazi kutokana na mashambulizi ya jeshi la Kizayuni na zaidi ya magari 100 ya kubebea wagonjwa yameharibiwa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Wanajeshi wa Israel wameichoma moto kwa makusudi Hospitali ya Kamal Adwan ili kuwanyima wakaazi wa eneo hili huduma za matibabu.

Asilimia kubwa ya majengo katika Ukanda wa Gaza yamebomelewa kufuatia hujuma ya kijeshi ya Israel

 

Wakati huo huo, Asim Iftikhar, balozi na mwakilishi wa Pakistan katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, hakuna sehemu yoyote duniani ambayo sheria za kimataifa za kibinadamu zinakanyagwa na kukiukwa kama ilivyo huko Gaza, na akabainisha kuwa kiwango cha kampeni hii ya mauaji ya kimbari ni cha kushangaza.

Nyumba, shule, hospitali na hata turathi za kitamaduni za Gaza zimeharibiwa. Hata Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wake hawajaachwa. Hii sio vita. Ni kampeni ya unyang'anyi, utokomezaji wa kizazi na uangamizaji, ulipuaji wa mabomu ovyo kwa raia na uharibifu ulioratibiwa wa miundombinu muhimu. Hizi ni hatua zilizopangwa zenye lengo la kuwafuta watu wote katika ardhi yao."

Suala jingine muhimu ni kwamba, licha ya ukosoaji wote wenye nyaraka wa wajumbe wa Baraza la Usalama kuhusiana na kuendelea mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza, Linda Thomas Greenfield, mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa aliunga mkono waziwazi mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza. Uungaji mkono huo wa Marekani ndio sababu kuu na muhimu ya kuendelezwa mauaji ya halaiki ya Wazayuni huko Gaza na kupuuzwa daghadagha na wasiwasi wote wa kimataifa kuhusiana na suala hilo.