Mamilioni ya watu nchini Afghanistan wanakabiliwa na uhaba wa Chakula
Maisha ya mamilioni ya raia nchini Afghanistan yapo hatarini kutokana na uhaba mkubwa wa chakula na ukosefu wa vifaa vya kukabiliana na baridi kali.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetoa limeeleza hofu yake kuhusu mzozo mbaya wa kibinadamu nchini Afghanistan, ambapo mamilioni ya familia zinakabiliwa na uamuzi wa kuhuzunisha wa kuchagua kati ya kuwalisha watoto wao au kuwaweka katika mazingiira ya joto wakati huuu wa baridi kali. Shirika hilo limetoa wito wa haraka wa msaada wa kimataifa ili kukabiliana na mzozo huo unaozidi kuongezeka.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeelezea wasiwasi wake mkubwa juu ya mzozo wa kiuchumi na kibinadamu nchini Afghanistan. Katika taarifa iliyosambazwa kwenye mtandao wa kijamii wa X siku ya Jumanne, shirika hilo liliangazia mapambano makali ya familia za Afghanistan, likibainisha kuwa wengi wanalazimika kuchagua kati ya chakula na kutumia pesa kwa kupasha joto ili kuishi.
WFP imesisitiza kuwa dola milioni 718 zinahitajika kutoa msaada muhimu kwa wale wanaohitaji katika kipindi cha miezi sita ijayo. Kulingana na tathmini ya shirika hilo, Waafghanistan milioni tano wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na hawana uhakika kuhusu mlo wao ujao utatoka wapi.
Jambo la kushangaza ni kwamba, milioni moja ya watu hawa wanaishi katika maeneo ya mbali na magumu kufikiwa, ikiwa ni pamoja na Badakhshan, Ghor, Bamyan, na Daikundi, ambapo hali mbaya ya hewa inazidisha changamoto za kutoa misaada.