Askari wa Kizayuni ashtakiwa Sweden kwa kushiriki katika vita vya Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121308-askari_wa_kizayuni_ashtakiwa_sweden_kwa_kushiriki_katika_vita_vya_gaza
Vyombo vya habari vya Kiebrania vimeripoti kuhusiana na kuwasilishwa  mashtaka dhidi ya mwanajeshi wa utawala wa Kizayuni huko nchini Sweden kutokana na kushiriki katika jinai za kivita huko Gaza.
(last modified 2025-01-11T10:11:50+00:00 )
Jan 11, 2025 10:11 UTC
  • Askari wa Kizayuni ashtakiwa Sweden kwa kushiriki katika vita vya Gaza

Vyombo vya habari vya Kiebrania vimeripoti kuhusiana na kuwasilishwa  mashtaka dhidi ya mwanajeshi wa utawala wa Kizayuni huko nchini Sweden kutokana na kushiriki katika jinai za kivita huko Gaza.

Katika siku za hivi karibuni kumewasilishwa mashtaka dhidi ya wanajeshi wa Israel katika nchi mbalimbali zikiwemo Brazil, Argentina na Sri Lanka jambo ambalo limezidisha wasi wasi wa utawala wa Kizayuni kuhusu kufuatiliwa kisheria wanajeshi wa Israel kote duniani.

Hivi karibuni askari wa jeshi la Kizayuni alitoroka kutoka Brazil baada ya mahakama moja nchini humo kuamuru polisi wa nchi hiyo kumchunguza mwanajeshi wa Israel aliyesafiri hadi katika nchi hiyo akituhumiwa kufanya uhalifu wa kivita huko Gaza. 

Kutokana kuongezeka wasi wasi wa utawala wa Kizayuni kuhusiana na kutiwa mbaroni askari wa utawala huo katika nchi mbalimbali duniani, vyanzo vya usalama vya utawala huo vimeonya kuhusiana na suala hilo.

Redio na Televisheni za Kizayuni zimeripoti kuwa, malalamiko 50 dhidi ya askari wa utawala huu yamesajiliwa katika nchi 10 za dunia.

Gazeti la Israel la Haaretz limeripoti: "Taasisi zinazofungamana na serikali zinajiandaa kuwasaidia wanajeshi ambao wanaweza kukamatwa au kufunguliwa mashtaka wakiwa safarini nje ya nchi kwa kuhusika na uhalifu wa kivita huko Gaza. Wanajeshi hao wa Kizayuni wamearifiwa juu ya kuangalia upya uamuzi wao wa kusafiri nje ya nchi na wakati huo huo, wanapaswa kutumia kwa kiwango kidogo mitandao ya kijamii.