Idadi ya watu waliouawa shahidi Gaza yapindukia 46,000
Idadi ya Wapalestina waliouawa shahidi tangu kuanza hujuma ya kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni huko Gaza (Oktoba 7, 2023) imepindukia mashahidi 46,000.
Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imetangaza kuwa, idadi ya mashahidi wa mashambulizi ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Ghaza imefikia 46,537.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, watu 46,537 wameuawa shahidi kutokana na mashambulizi ya jeshi la Israel kwenye Ukanda wa Gaza tangu tarehe 7 Oktoba mwaka 2023.
Pia, taasisi hiyo ya matibabu ya Palestina imesema kuwa, jumla ya watu waliojeruhiwa kutokana na mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza vita katika ukanda huo imefikia watu 109,571.
Aidha Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Ghaza imetangaza kuwa, katika muda wa saa 24 zilizopita, Jeshi la Kizayuni limefanya jinai na mauaji 5 katika Ukanda wa Ghaza.
Uungaji mkono wa wazi wa Marekani na nchi za Magharibi umepelekea kushuhudiwa faili jeusi la viongozi watenda jinai wa utawala wa Kizayuni wanaoua watu wasio na ulinzi wala hatia. Bila shaka wale wote wanaohami na kuunga mkono jinai za Israel wanahusika pia katika jinai na mauaji ya kimbari ya utawala huo katika Ukanda wa Gaza.