Al-Houthi: Wazayuni ni nembo ya unyama na ukatili
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121320-al_houthi_wazayuni_ni_nembo_ya_unyama_na_ukatili
Muhammad Ali al-Houthi mmoja wa viongozi waandamizi wa Haarakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, utawala haramu wa Israel ni nembo ya wazi kabisa ya unyama na ukatili.
(last modified 2025-01-11T23:32:18+00:00 )
Jan 11, 2025 23:32 UTC
  • Al-Houthi: Wazayuni ni nembo ya unyama na ukatili

Muhammad Ali al-Houthi mmoja wa viongozi waandamizi wa Haarakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, utawala haramu wa Israel ni nembo ya wazi kabisa ya unyama na ukatili.

Al-Houthi amesema hayo katika radiamali yake kwa uchokozi wa utawala wa Kizayuni na Marekani huko Yemen na kuwahututubu akisisitiza kwamba, "Nyinyi ni nembo ya wazi ya jinai na ukatili."

Kwa mujibu wa ripoti ya mtandao wa al-Masirah huko Yemen, al-Houthi alisisitiza: Taarifa zenu (mamlaka za Israel) zenye kupingana na kuchanganyikiwa sio tu kwamba hazitutishi, bali pia zinawafanya mashujaa wa Yemen waazimie zaidi kuendelea kuiunga mkono Gaza na kuangamiza utawala unaotenda jinai kkila uchao wa Israel.

Muhammad Ali al Houthi ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amebainisha kuwa, mashambulizi dhidi ya Yemen yanatokana na hatua ya wananchi wake kuunga mkono Gaza.

Aidha amesema, hujuma dhidi ya Yemen zimeimarisha imani na azma ya watu wetu katika mapambano dhidi ya ugaidi na mauaji ya halaiki ya adui Mzayuni.

Wakati huo huo, walimwengu wameendelea kulaani udhaifu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusiana na kuendelea mauaji ya halaiki huko Ghaza na hujuma za kijeshi za Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni katika miundombinu muhimu ya Yemen, na kueleza kuwa, taasisi hiyo inashindwa waziwazi kutekeleza majukumu yake ya kusimamisha unyama wa utawala wa Kizayuni.