Nini madhumuni ya kuzidisha mashambulizi dhidi ya Yemen?
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121346-nini_madhumuni_ya_kuzidisha_mashambulizi_dhidi_ya_yemen
Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mara nyingine tena zimeanzisha mashambulizi ya pamoja na makali dhidi ya Yemen.
(last modified 2025-01-12T09:09:15+00:00 )
Jan 12, 2025 09:09 UTC
  • Nini madhumuni ya kuzidisha mashambulizi dhidi ya Yemen?

Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni wa Israel kwa mara nyingine tena zimeanzisha mashambulizi ya pamoja na makali dhidi ya Yemen.

Mashambulizi yaliyofanywa na Marekani na Uingereza Alkhamisi iliyopita yalilenga vituo vya kuhifadhia silaha kusini mwa Sanaa na katika jimbo la Amran kaskazini mwa Yemen. Katika kukabiliana na mashambulizi hayo, Jeshi la Yemen limeshambulia ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina kwa kutumia ndege tatu zisizo na rubani. Jeshi la Israel pia lilitangaza katika taarifa yake siku ya Ijumaa kwamba ndege zake za kivita zimeshambulia taasisi na miundombinu ya kijeshi kwenye kituo cha Hazaz na miundombinu ya kijeshi katika Bandari ya Hudaydah na Ras Issa kwenye pwani ya magharibi na ndani ya Yemen.

Ijumaa iliyopita pia, Redio ya Jeshi la Israel ilithibitisha kuwa utawala huo umefanya mashambulizi dhidi ya Yemen na kutangaza kuwa, Jeshi la Anga la Israel liliishambulia Yemen kwa ndege 20 za kivita. Chombo hicho cha habari cha Kizayuni kilitangaza kuwa vikosi hivyo vililenga maeneo matatu muhimu kwa kurusha zaidi ya mabomu 50.

Mashambulizi ya Marekani na washirika wake dhidi ya Yemen

Mashambulizi hayo yanaashiria kuwa Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni zimejikita zaidi katika suala la Yemen. Yemen iliingia vitani siku 40 baada ya utawala wa kibaguzi wa Israel kuanza mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza, kwa kushambulia meli zinazohusishwa na utawala huo. Yemen imekuwa ikizuia meli za mizigo kuelekea bandari za Israel kwa kuzishambulia na kuzidisha gharama za kiuchumi za utawala wa Kizayuni katika vita dhidi ya Gaza, jambo ambalo limekuwa na mafanikio makubwa.

Nukta nyingine ni kuwa, Marekani na Uingereza, zilichukua jukumu la kukabiliana na Yemen ili kuunga mkono na kuuhami utawala wa Kizayuni wa Israel na zimekuwa zikifanya mashambulizi ya mara kwa mara dhidi Yemen. Hata hivyo, mashambulio hayo sio tu kwamba hayakuwazuia Wayemeni kushambulia meli zinazoelekea katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu ya Palestina, bali katika kujilinda, Wayemeni wamefanya mashambulizi dhidi ya manuwari za kubeba ndege za kivita za Marekani, meli za Marekani na Uingereza, na naeneo mbalimbali ya Israel.

Taarifa ya jeshi la Yemen imesema: "Tumelenga manuwari ya ndege za kivita ya Marekani, USS Harry Truman, na meli kadhaa za kivita kaskazini mwa Bahari Nyekundu kwa idadi kadhaa ya makombora na ndege zisizo na rubani." Taarifa hiyo iliongeza kuwa operesheni hiyo ilizima shambulio jipya la anga la adui, ambalo lilipangwa kufanywa kutoka kwenye manuwari USS Harry Truman, na kuilazimisha kuondoka katika maji ya eneo la kaskazini la Bahari Nyekundu.

Kuna nukta kadhaa muhimu za kuzingatiwa kuhusu mashambulizi hayo ya Marekani, Uingereza na utawala wa Kizayuni dhidi ya Yemen.

Nukta ya kwanza ni kwamba, Marekani na Uingereza na vilevile utawala unaoikalia kwa mabavu Quds tukufu, hazikuwa na tathmini sahihi kuhusu uwezo wa kijeshi wa Wayemeni. Kwa mantiki hiyo, weledi wa mambo wanaamini kuwa, operesheni isiyo na kifani ya Jeshi la Yemen, mbali na kuzuia juhudi za Marekani na Uingereza za kuvunja mzingiro wa jeshi la majini dhidi ya Israel, imedhihirisha nguvu za kijeshi ambazo Washington ilikuwa haizijui, na kwa hakika imevuruga milingano ya nvugu.

Nukta ya pili ni kwamba, Marekani, Uingereza na Israel zinataka kutengeneza "Syria mpya" huko Yemen kupitia mashambulizi yao. Mashambulizi yanayofanywa dhidi ya miundombinu ya Yemen, haswa mitambo ya umeme, pia yanafanyika kwa lengo hilo. Kwa hakika, lengo lao ni kuzusha hali ya kutoridhika kwa umma, na hivyo kufungua njia ya migogoro ya ndani nchini Yemen na hatimaye serikali mjini Sanaa kupoteza uungwaji mkono wa umma. Hata hivyo, njama hiyo pia inatajwa kuwa ni kosa la kimahesabu, kwa sababu baada ya mashambulizi hayo mamia ya maelfu ya Wayemeni walifanya maandamano makubwa ya kuunga mkono serikali na kuwatetea wananchi wa Palestina.

Maandamano ya watu wa Yemen dhidi ya Marekani, na Israel

Nukta ya tatu ya kuzingatiwa ni kwamba mashambulizi hayo mfululizo hayakuweza kuwawazuia Wayemeni kuwatetea watu wa Gaza. Kwa msingi huo, taarifa ya Jeshi la Yemen imesema: "Tunaendelea kutilia mkazo wajibu wetu wa kuwatetea watu wanaodhulumiwa wa Palestina, na operesheni zetu hazitasimama kamwe isipokuwa hujuma za utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza na mzingiro wake vitakapokomeshwa.