Israel yasalimu amri baada ya kushindwa kuiangamiza HAMAS
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121498-israel_yasalimu_amri_baada_ya_kushindwa_kuiangamiza_hamas
Baada ya mapigano ya miezi 15 huko Ghaza hatimaye utawala wa Kizayuni wa Israel umelazimika kusalimu amri na kukubali makubaliano ya kusitisha mapigano bila ya kufanikiwa kuiangamiza Hamas wala kokomboa mateka wa Kizayuni.
(last modified 2026-05-20T03:07:53+00:00 )
Jan 16, 2025 04:07 UTC
  • Israel yasalimu amri baada ya kushindwa kuiangamiza HAMAS

Baada ya mapigano ya miezi 15 huko Ghaza hatimaye utawala wa Kizayuni wa Israel umelazimika kusalimu amri na kukubali makubaliano ya kusitisha mapigano bila ya kufanikiwa kuiangamiza Hamas wala kokomboa mateka wa Kizayuni.

Shirika la habari la FARS limeandika makala inayosema kuwa, utawala wa Kizayuni ambao umeshindwa kufikia hata lengo lake moja ulilokuwa umelitangaza wakati ilipoanzisha mashambulizi ya kikatili dhidi ya Ghaza miezi 15 iliyopita, hatimaye imesalimu amri na kukubali kusitisha vita na kubadilishana mateka na HAMAS.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Mohammed bin Abdulrahman Aal Thani ametangaza hilo rasmi mbele ya waandishi wa habari na kuthibitishwa pia na duru za Palestina na za utawala wa Kizayuni. 

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, makubaliano hayo ya kusitisha vita yamepangwa kuanza kutekelezwa rasmi siku ya Jumapili.

Makubaliano haya yamekuja wakati ambapo, kwa mujibu wa mashirika ya usalama ya Israel, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imeweza kujenga upya uwezo wake wa kivita katika miezi ya hivi karibuni na kila siku inafanya mashambulizi na kuwatia hasara wanajeshi wa Israel huko Ghaza.

Mwezi Oktoba 2023, wanamapambano wa Palestina wakiongozwa na HAMAS waliendesha operesheni ya kishujaa na kuyatia aibu ya kihistoria mashirika ya kijasusi na kiusalama ya Israel. Hiyo ilikuwa ni operesheni na Kimbunga cha al Aqsa ambayo haiwezi kufutika katika historia.

Tangu wakati huo utawala wa Kizayuni umekuwa ukifanya mauaji ya kinyama dhidi ya wananchi madhlumu wa Palestina lakini imeshindwa kukomboa mateka wa Kizayuni wala kuingamiza harakati ya HAMAS.