Abu Sharif: Wananchi wa Gaza wamezuia ushindi wa utawala wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i121596-abu_sharif_wananchi_wa_gaza_wamezuia_ushindi_wa_utawala_wa_israel
Mwakilishi wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina mjini Tehran amesema: Licha ya uchache wa suhula waliokuwa nao, wananchi wa Gaza waliweza kuendeleza mapambano yao ya ukombozi na kuzuia kusonga mbele utawala wa Kizayuni kutokana na uungaji mkono na msaada mkubwa wa Mhimili wa Muqawama unaojumuisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Lebanon, Iraq na Yemen.
(last modified 2025-01-18T07:28:54+00:00 )
Jan 18, 2025 07:28 UTC
  • Nasser Abu Sharif
    Nasser Abu Sharif

Mwakilishi wa harakati ya Jihad Islami ya Palestina mjini Tehran amesema: Licha ya uchache wa suhula waliokuwa nao, wananchi wa Gaza waliweza kuendeleza mapambano yao ya ukombozi na kuzuia kusonga mbele utawala wa Kizayuni kutokana na uungaji mkono na msaada mkubwa wa Mhimili wa Muqawama unaojumuisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Lebanon, Iraq na Yemen.

Nasser Abu Sharif amesema leo katika mkutano wa "Gaza Nembo ya Muqawama" kwamba: Vita vingali vinaendelea na utawala wa Kizayuni na tunapasa kutambua kuwa kuna mamilioni ya vitendo visivyo vya kibinadamu na kinyume na maadili katika rekodi ya utendaji ya utawala huo. 

Mwakilishi wa Jihad Islami ya Palestina mjini Tehran amesema: Bado wapo waungaji mkono wa utawala wa Israel zikiwemo Marekani na Ulaya na katika kipindi cha miezi 15 iliyopita tumeshudia kukanyagwa na kupuuzwa aghalabu ya thamani na sheria za kibinadamu kwa sababu ya kuuhami na kuunga mkono utawala wa Kizayuni au hata kuzishinikiza mahakama za kimataifa kwa sababu zimeulani utawala huo ghasibu. 

Abu Sharif ameongeza kuwa: Watu wa Palestina wameendeleza mapambano ya ukombozi licha ya mauaji makubwa na uharibifu uliofanywa na Israel; na njia hiyo itaendelewa, na inshaallah kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, Wapalestina wataibuka na ushindi dhidi ya adui Mzayuni.