Hizbullah yapinga madai ya kuhusika na shambulio la maroketi
(last modified Sun, 23 Mar 2025 02:48:18 GMT )
Mar 23, 2025 02:48 UTC
  • Hizbullah yapinga madai ya kuhusika na shambulio la maroketi

Baada ya utawala wa Israel kudai kwamba maroketi 5 yalirushwa kuelekea katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu jana Jumamosi, Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imekanusha kuhusika kivyovyote na shambulio hilo.

Katika taarifa yake Jumamosi alasiri, Hizbollah imekanusha kuhusika kwa namna yoyote na kuvurumishwa roketi kutoka kusini mwa Lebanon hadi maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, tovuti ya televisheni ya Al Manar imeripoti.

Harakati hiyo ya Muqawama ya Lebanon imeendelea kusema kuwa "inafngamana na ahadi yake ya kusimamisha vita na inasimama nyuma ya taifa la Lebanon katika kukabiliana na hatua ya Wazayuni kushadidisha taharuki dhidi ya Lebanon."

"Madai ya adui wa Israel yanalenga kuhalalisha mashambulizi ya mara kwa mara dhidi ya Lebanon ambayo hayajasimama tangu kutangazwa kwa usitishaji vita," taarifa ya Hizbullah imebainisha zaidi.

Utawala wa Kizayuni wa Israel uulianzisha mashambulizi kadhaa kusini mwa Lebanon baada ya kuibua madai ya kurushwa maroketi matano ambayo ulisema yalinaswa.

Mwandishi wa Al-Manar wa Lebanon aliripoti kuwa raia wawili waliuawa shahidi, wengine 3 walijeruhiwa katika shambulio la Israeli kwenye mji wa kusini wa Touline. Anasema kuwa adui Mzayuni amefanya mashambulizi 20 katika miji ya kusini mwa Lebanon.