Waziri Mkuu wa zamani wa Israel akiri juu ya uhaba mkubwa wa askari jeshini
Naftali Bennet Waziri Mkuu wa zamani wa utawala wa Kizayuni amekiri kuwa jeshi la utawala huo linakabiliwa na uhaba mkubwa wa askari jeshini.
Amesema, haijawahi kutokea hali kama hii ambapo Israel inahitaji idadi kubwa ya wanajeshi jeshini.
Gazeti la Kizayuni la Yediot Aharonoth pia limeandika katika ripoti yake kuwa: Uhaba mkubwa wa askari jeshi umesababishwa na vita vya muda mrefu katika Ukanda wa Gaza na kulilazimisha jeshi la utawala huo kuongeza muda wa tahadhari.
Televishei ya Kan ya utawala wa Kizayuni pia iliwahi kuzungumzia uhaba wa askari jeshi katika jeshi la Israel.
Televisheni hiyo inayorusha matangazo kwa lugha ya Kiibrania ilieleza kuwa jeshi la Israel limewatuma katika uwanja wa vita huko Gaza wanajeshi wapya wa vikosi viwili vya Goolan na Guhati bila hata ya kuwapa mafunzo.
Wanajeshi hao waliajiriwa miezi minne iliyopita na kupelekwa kwenye uwanja wa vita bila kupata mafunzo muhimu.