UNICEF: Israel imeua watoto 45 wauawa Gaza kwa muda wa siku mbili
Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto (UNICEF) umetangaza kuwa, wanajeshi wa Israel wamewaua shahidi watoto 45 katika Ukanda wa Gaza ndani ya siku mbili.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limetangaza kuwa, wanajeshi wa Israel wameua watoto 45 katika Ukanda wa Gaza katika muda wa siku mbili zilizopita. Huu ni ukumbusho mwingine wa kutisha kwamba watoto huko Gaza ndio wa kwanza kuteseka. Wanakabiliwa na njaa kila siku na kisha kuwa waathirika wa mashambulizi ya kiholela.
Shirika la Afya Duniani pia lilitangaza kwamba mashambulizi ya Israel yanaendelea kuathiri vituo vya matibabu, ikiwa ni pamoja na Hospitali ya Ulaya ya Gaza huko Khan Younis, ambayo imefungwa. Kufungwa kwa hospitali hii kumewanyima wagonjwa huduma muhimu wakiwemo wagonjwa wa moyo, saratani na ubongo. Kufungwa kwa hospitali hii kutaongeza shinikizo kwenye mfumo wa matibabu.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, asasi mbalimbali za kimataifa zimeendelea kuonya kuhusiana na hali mbaya ya uhaba na ukosefu wa chakula katika Ukanda wa Gaza na kueleza kuwa, hivi sasa maghala ya chakula katika ukanda huo yapo tupu.
Mashirika ya kimataifa hayo ya yametangaza kuwa, chakula chote katika Ukanda wa Gaza kimeisha, na kueleza kwamba, maafa ya kibinadamu katika Ukanda huo yamefikia kiwango cha maafa na sasa eneo hilo liko katika hatua ya njaa halisi.