Hizbullah: Israel ilitaka kuisambaratisha Iran, lakini Tehran ikaibuka mshindi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i128496
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala wa Israel ulikuwa ukitaka kuendeleza ajenda yake ya uharibifu dhidi ya Iran wakati wa vita vyake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu mwezi uliopita, lakini Tehran iliweza kuushinda utawala huo ghasibu.
(last modified 2025-07-19T06:48:26+00:00 )
Jul 19, 2025 04:46 UTC
  • Hizbullah: Israel ilitaka kuisambaratisha Iran, lakini Tehran ikaibuka mshindi

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema utawala wa Israel ulikuwa ukitaka kuendeleza ajenda yake ya uharibifu dhidi ya Iran wakati wa vita vyake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu mwezi uliopita, lakini Tehran iliweza kuushinda utawala huo ghasibu.

Sheikh Naim Qassem alisema hayo wakati wa hotuba yake jana Ijumaa na kueleza kuwa, "Vita hivyo vilianzishwa kwa kisingizio cha kukabiliana na shughuli za nyuklia za Iran."

Utawala wa Israel ulianzisha vita dhidi ya Iran tarehe 13 Juni, vikilenga vituo vya nyuklia vya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na miundombinu mingine pamoja na maafisa mbalimbali na raia wa kawaida.

Sheikh Qassem amebainisha kuwa utawala huo ulianzisha vita hivyo, huku wakaguzi wote wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) wamethibitisha hali ya amani ya shughuli za nishati ya nyuklia za Jamhuri ya Kiislamu.

Mkuu wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon ameeleza bayana kuwa, "Kwa hivyo, ilionekana wazi kuwa lengo la kweli la Israeli lilikuwa kuiangamiza Iran, lakini Tehran ilifanikiwa kupata ushindi."

Afisa huyo alikuwa akiashiria operesheni iliyofanikiwa ya Vikosi vya Majeshi ya Iran katika kujihami na kulipiza kisasi katika muda wote wa uchokozi huo, ambapo Tel Aviv baada ya kusakamwa, illtoa wito wa kusitishwa mapigano baada ya siku 12.