Amnesty yaitaka Israel imuachie huru Mpalestina aliyesusia chakula
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i13156-amnesty_yaitaka_israel_imuachie_huru_mpalestina_aliyesusia_chakula
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeutaka utawala haramu wa Israel umuachie huru mfungwa wa Kipalestina Bilal Kayed ambaye amekuwa katika mgomo wa chakula kwa miezi miwili sasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 12, 2016 23:20 UTC
  • Amnesty yaitaka Israel imuachie huru Mpalestina aliyesusia chakula

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeutaka utawala haramu wa Israel umuachie huru mfungwa wa Kipalestina Bilal Kayed ambaye amekuwa katika mgomo wa chakula kwa miezi miwili sasa.

Taarifa iliyotolewa na Amnesty International jana Ijumaa imesema kuwa, iwapo utawala wa Kizayuni wa Israel una ushahidi kuwa Mpalestina huyo mwenye umri wa miaka 35 ametenda jinai ya aina yoyote, basi umfungulie mashtaka mara moja, la sivyo umuchie huru. Kayed ambaye ni mwanachama wa harakati ya Popular Front for the Liberation of Palestine, alikamatwa na wanajeshi katili wa Israel mwaka 2002 na amekuwa katika jela za utawala huo ghasibu kwa zaidi ya miaka 14 na nusu sasa.

Maaandamano ya kushinikiza kuachiwa huru Bilal Kayed

Mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu, Jumuiya ya Wafungwa wa Kipalestina katika Jela za Israel (PPS) ilitangaza kuwa mahabusu 60 wa Kipalestina walikataa kula chakula katika gereza la Megiddo huko kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, kupinga uamuzi wa mamlaka ya magereza ya utawala haramu wa Israel wa kuendelea kumfunga Bilal Kayed bila ya kufunguliwa mashtaka.

Moja ya jela za utawala haramu wa Israel

Wapalestina zaidi ya 7,500 wanashikiliwa katika korokoro za kutisha za Israel katika mazingira mabaya yanayokosolewa mara kwa mara na jumuiya nyingi za kutetea haki za binadamu.