Israel yaendelea kukanyaga makubaliano ya kusitisha vita Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i132956-israel_yaendelea_kukanyaga_makubaliano_ya_kusitisha_vita_ghaza
Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kukanyaga makubaliano ya kusimamisha vita Ghaza na umefanya mashambulizi mapya dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa ukanda huo iliouzingira kila upande.
(last modified 2025-11-09T02:39:58+00:00 )
Nov 09, 2025 02:39 UTC
  • Israel yaendelea kukanyaga makubaliano ya kusitisha vita Ghaza

Utawala wa Kizayuni wa Israel unaendelea kukanyaga makubaliano ya kusimamisha vita Ghaza na umefanya mashambulizi mapya dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa ukanda huo iliouzingira kila upande.

Jeshi la Israel limefanya mashambulizi mapya ya anga katika maeneo ya Khan Younis na Rafah ya kusini mwa Ukanda wa Ghaza huku matingatinga ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni yakibomoa majengo zaidi ya raia, kwenye jiji la Ghaza. Mashambulizi hayo yamefanywa na Israel licha ya kuweko mwito wa kimataifa wa kuutaka utawala wa Kizayuni ukomeshe jinai zake na uruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Ghaza.

Mashambulio mapya ya jeshi la Israel yameendelea kuharibu miundombinu muhimu na kuzidi kuzisababishia matatizo familia za Wapalestina zilizopoteza makazi yao kwenye mashambulizi ya kikatili ya miaka miwili ya Israel. Mashambulizi ya walowezi wa Kizayuni nayo yameongezeka na kufika hadi Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Umoja wa Mataifa umesema kuwa, asilimia 92 ya majengo ya makazi ya raia huko Ghaza yameharibiwa au kubomolewa kabisa katika mashambulizi ya kinyama ya Israel yaliyodumu kwa miaka miwili. Umoja huo umeripoti pia kwamba mashambulizi haramu ya Wazayuni yamefikia kiwango cha kutisha kiasi kwamba Wizara ya Afya ya Ghaza imesema kwamba, zaidi ya Wapalestina 240 wameuawa tangu Oktoba 10 licha ya kuwepo makubaliano rasmi ya kusitisha mapigano.

Wataalamu wanasema kwamba makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Marekani hayajaleta mabadiliko yoyote kwa Wapalestina, kwani mashambulizi ya kila siku yanaendelea kufanywa utawala wa Kizayuni ambao pia unaendelea kuzuia kuingia Ghaza misaada ya kibinadamu, tofauti ya ilivyokubaliwa kwenye mapatano ya Sharm Sheikh, Misri, yaliyomaliza vita vya miaka miwili vilivyoanzishwa na Israel dhidi ya Ghaza.