Jeshi la Afghanistan: Tumemuua kamanda mkubwa wa kundi la Taleban
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i15766-jeshi_la_afghanistan_tumemuua_kamanda_mkubwa_wa_kundi_la_taleban
Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Afghanistan imetangaza kuuawa mmoja wa makamanda wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Taleban.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 21, 2016 04:13 UTC
  • Jeshi la Afghanistan: Tumemuua kamanda mkubwa wa kundi la Taleban

Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Afghanistan imetangaza kuuawa mmoja wa makamanda wa ngazi za juu wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Taleban.

Kwa mujibu wa wizara hiyo, Mawlawi Muawiyah, mmona wa vinara mashuhuri na wa ngazi ya juu wa kundi hilo maarufu kwa kutenda jinai dhidi ya binaadamu ndani na nje ya nchi hiyo, ameangamizwa katika shambulio la maafisa usalama katika mkoa wa Kunduz nchini humo. Wizara ya Mambo ya Ndani nchini Afghanistan imesema kuwa jana ndege za kijeshi za nchi hiyo ziliyalenga maficho ya wanachama wa genge hilo latika wilaya ya Dashti Archi mkoani hapo.

Wanachama wa Taleban

Katika shambulizi hilo, mbali na Mawlawi Muawiyah, wanachama wengine 22 wa kundi hilo waliuawa. Itafahamika kuwa, kiongozi huyo wa Taleban, alikuwa na nafasi muhimu sana katika kuratibu mashambulizi ya kigaidi katika mkoa wa Kunduz na kuua raia wengi wa nchi hiyo kupitia miripuko ya mabomu.