Tunisia kuwa mwenyeji wa kikao cha kimataifa kuhusu Libya
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i18469-tunisia_kuwa_mwenyeji_wa_kikao_cha_kimataifa_kuhusu_libya
Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia imeeleza kwamba nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa kikao cha kimataifa cha kujadili mgogoro wa Libya mapema mwakani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 31, 2016 00:54 UTC
  • Tunisia kuwa mwenyeji wa kikao cha kimataifa kuhusu Libya

Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia imeeleza kwamba nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa kikao cha kimataifa cha kujadili mgogoro wa Libya mapema mwakani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Tunisia imetangaza kuwa kundi lal nchi zitakazoshiriki kwenye kikao hicho linaloundwa na nchi 5 za kaskazini mwa Afrika na 5 za kusini magharibi mwa eneo la Mediterania zimekubali pendekezo la Tunisia la kuwa mwenyeji wa kikao hicho cha kimataifa kilichopangwa kufanyika mapema mwakani ili kuchunguza hali ya mambo ya Libya.

Magaidi wa Daesh na hujuma zao nchini Libya

Kundi hilo linalojulikana kwa jina la 5+5 linaundwa na nchi za Muungano wa Maghreb Arabi yaani Tunisia, Libya, Algeria, Morocco na Mauritania na pia nchi za kaskazini magharibi mwa eneo la Mediterania yaani Italia, Ufaransa, Malta, Uhispania na Ureno. 

Libya imetumbukia katiak dimbwi la machafuko tangu alipopinduliwa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muamar Gaddafi  mwaka 2011, na nchi hiyo sasa imegeuzwa kuwa mahali pa harakati za kundi la kigaidi la Daesh.