Iraq: Tumeazimia kuliangamiza kikamilifu kundi la kigaidi la Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i25836-iraq_tumeazimia_kuliangamiza_kikamilifu_kundi_la_kigaidi_la_daesh
Serikali ya Iraq imetangaza kuwa, imeazimia kuliangamiza kikamilifu kundi la kigaidi la Daesh na kwamba, vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vinaendelea vizuri na operesheni zake dhidi ya wanamgambo hao wa kigaidi.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Mar 02, 2017 04:44 UTC
  • Iraq: Tumeazimia kuliangamiza kikamilifu kundi la kigaidi la Daesh

Serikali ya Iraq imetangaza kuwa, imeazimia kuliangamiza kikamilifu kundi la kigaidi la Daesh na kwamba, vikosi vya ulinzi vya nchi hiyo vinaendelea vizuri na operesheni zake dhidi ya wanamgambo hao wa kigaidi.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Iraq ambaye amesisitiza kuwa, lengo la serikali ya nchi hiyo ni kuliangamiza kikamilifu kundi la Daesh na kulifuta katika ardhi ya nchi hiyo hususan katika mji wa Mosul/

Qasim Mohammad Jalal al-'Araji amesema hayo wakati alipoutembea mji wa Mosul ambapo sambamba na kuashiria juu ya kufungamana vikosi vya nchi hiyo na suala la kuheshimu haki za binadamu na upande wa kiutu ameongeza kuwa, kutokana na vikosi vya nchi hiyo kusonga mbele katika operesheni zake dhidi ya magaidi wa Daesh muda si mrefu mji wa Mosul utakombolewa na kuondoka chini ya udhibiti wa kundi hilo la kitakfiri.

Wanachama wa Daesh

Hivi sasa vikosi vya ulinzi vya Iraq vikiwa na lengo la kuwatenganisha magaidi na Daesh na raia wa kawaida limeanza mwenendo mrefu wa kuainisha utambulisho katika mji wa Mosul.

Operesheni ya kulikomboa eneo la magharibi mwa Mosul kutoka katika makucha ya wanachama wa genge la kigaidi la Daesh zilianza hivi karibuni kwa amri ya Waziri Mkuu wa Iraq, Haider al-Abadi. 

Hii ni katika hali ambayo mwezi uliopita pia jeshi la Iraq kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Hashdu sh-Shaab lilifanikiwa kuyakomboa maeneo ya mashariki mwa mji huo wa Mosul na kuwafanya maelfu ya wakazi wa meneo hayo kurejea makwao.