Wanajeshi wa Israel wamkamata mbunge mwanamke Mpalestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i26180-wanajeshi_wa_israel_wamkamata_mbunge_mwanamke_mpalestina
Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamewakamata Wapalestina kadhaa akiwemo mbunge mwanamke.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 10, 2017 04:02 UTC
  • Wanajeshi wa Israel wamkamata mbunge mwanamke Mpalestina

Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamewakamata Wapalestina kadhaa akiwemo mbunge mwanamke.

Mjumbe wa Bunge la Palestina Bi. Samira al Halayka ambaye ni mwanachama wa Hamas, alikamatwa  Alhamisi akiwa nyumbani kwake katika mji wa al-Shoyoukh katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Duru zinadokeza kuwa mbunge huyo alifungwa pingu kisha akafunikwa macho na kupelekwa kusikojulikana na wanajeshi hao wa Israel.

Taarifa zinasema wanajeshi wa Israel pia walipora kompyuta yake na simu yake ya mkononi katika oparesheni hiyo ya utekaji nyara.

Askari wa Israel wakimkamata Mpalestina

Baada ya kutekwa nyara al Halayka, idadi ya wabunge wa Palestina wanaoshikiliwa katika korokoro za Israel imeongezeka na kufika 10.

Kwa ujumla kuna Wapalestina karibu 7,000 katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel.