Maulamaa Bahrain wasema ni wadhifa wa kidini kumtetea Sheikh Issa Qassim
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i26358-maulamaa_bahrain_wasema_ni_wadhifa_wa_kidini_kumtetea_sheikh_issa_qassim
Maulamaa wa Kiislamu nchini Bahrain wametoa taarifa na kusema, ni wadhifa wa kidini na kitaifa kumtetea Ayatullah Sheikh Issa Qassim, kiongozi wa kimaanawi wa harakati wa mapinduzi ya wananchi.
(last modified 2026-03-27T07:58:19+00:00 )
Mar 14, 2017 01:10 UTC
  • Maulamaa Bahrain wasema ni wadhifa wa kidini kumtetea Sheikh Issa Qassim

Maulamaa wa Kiislamu nchini Bahrain wametoa taarifa na kusema, ni wadhifa wa kidini na kitaifa kumtetea Ayatullah Sheikh Issa Qassim, kiongozi wa kimaanawi wa harakati wa mapinduzi ya wananchi.

Katika taarifa Jumatatu, Maulamaa wameongeza kuwa kuwa, "Leo Bahrain imefika katika kipindi ambacho, madhalimu na maadui wameungana pamoja kwa ajili ya kuwahujumu wananchi, dini, madhehebu na viongozi wa wa kidini."

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, taifa la Bahrain lenye kupambana na kusimama kidete linaweza kujisimamia hata katika hali ngumu zaidi na litaendeleza mapambano hadi kupata ushindi mbele  ya mfumo wa kibaguzi wa ukoo wa Aal Khalifa.

Tarehe 27 Februari kesi ya Sheikh Issa Qassim iliakhirishwa tena kutokana na hofu ilionao utawala wa Aal Khalifa kuhusu majibu makali ya wananchi endapo mwanazuoni huyo maarufu wa Kiislamu atahukumiwa.

Maandamano ya kumuunga mkono Sheikh Issa Qassim

Kesi hiyo iliahirishwa hadi leo14 Machi, siku ambayo  inasadifiana na kuingia wanajeshi vamizi wa Bahrain nchini humo kwa lengo la kuwakandamiza wananchi wanamapinduzi.

 Wizara ya Mambo ya Ndani ya Bahrain inadai kuwa Sheikh Issa Qassim anahudumia madola ajinabi na kuibua hitilafu za kimadhehebu na kwa msingi huo Juni 20 mwaka jana ulimpokonya uraia. Sheikh Qassim amekanusha tuhuma hizo na kuzitaja kuwa zisizo na msingi.