Israel yakiri kuongezeka harakati ya ususiaji dhidi yake duniani
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i26654-israel_yakiri_kuongezeka_harakati_ya_ususiaji_dhidi_yake_duniani
Vyombo vya habari vya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, vimetangaza ongezeko kubwa la 'Harakati ya Ulimwengu ya Ususiaji dhidi ya Israel' maarufu kwa jina la BDS.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 21, 2017 00:38 UTC
  • Israel yakiri kuongezeka harakati ya ususiaji dhidi yake duniani

Vyombo vya habari vya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, vimetangaza ongezeko kubwa la 'Harakati ya Ulimwengu ya Ususiaji dhidi ya Israel' maarufu kwa jina la BDS.

Gazeti la Israel la lugha ya Kiebrania la Jumatatu ya jana sambamba na kuandika habari hiyo, limesisitiza kuwa, ongezeko hilo la harakati ya ususiaji dhidi ya Israel imeshika kasi zaidi hivi sasa duniani ikiwemo Italia na kwamba mwenendo huo ni tishio halisi kwa Tel Aviv.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni akiwa amechanganyikiwa

Sambamba na kuashiria ongezeko la harakati hiyo hata baina ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini Italia, gazeti hilo limeongeza kuwa, mwanzoni mwa mwezi huu, Baraza la Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Torino nchini Italia lilitangaza uungaji wake mkono juu ya pendekezo la kusitishwa ushirikiano na taasisi ya Technion ya utawala wa Kizayuni. Kwa mujibu wa gazeti hilo, mbali na hayo, ukumbi wa mkutano wa Chuo Kikuu cha La Sapienza mjini Roma, ulikuwa uwanja wa upashaji habari zilizowaonyesha askari wa Israel wakiwashambulia raia madhlumu wa Palestina na kupora ardhi zao asili.

Askari wa utawala wa Kizayuni akiwashambulia wanawake wa Kipalestina bila huruma

Kadhalika gazeti hilo limedai kwamba, harakati ya ususiaji dhidi ya utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, inafanya juhudi za kuwaonyesha Mayahudi kuwa ndio chanzo cha shari duniani. Wakati huo huo, gazeti la Kizayuni la Yedioth Aharonot limefichua kuwa, hivi karibuni jumuiya za wahisani nchini Chile, zilisusia kumualika mke wa balozi wa Israel katika kikao cha kila mwaka cha wahisani nchini humo, suala ambalo limeitia wasi wasi mkubwa Tel Aviv.

Harakati ya ususiaji dhidi ya Israel BDS

Gazeti la Yedioth Aharonot limesema kuwa, kutoalikwa mke wa balozi wa Israel katika kikao hicho cha udiplomasia, kumetokana na harakati za BDS, zinazosisitizia umuhimu wa kuususia utawala wa Israel. Harakati ya BDS ilianzisha harakati zake dhidi ya Israel miaka miwili iliyopita.