Bahrain yamfunga miaka 10 jela mbunge wa zamani wa al-Wefaq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i27014-bahrain_yamfunga_miaka_10_jela_mbunge_wa_zamani_wa_al_wefaq
Vyombo vya mahakama nchini Bahrain vimeendeleza wimbi la hukumu zake zisizo za kiadilifu dhidi ya wanaharakati na wakosoaji wa utawala wa Aal-Khalifa, baada ya kutoa hukumu ya vifo na kifungo jela kwa wanaharakati kadhaa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 29, 2017 09:24 UTC
  • Bahrain yamfunga miaka 10 jela mbunge wa zamani wa al-Wefaq

Vyombo vya mahakama nchini Bahrain vimeendeleza wimbi la hukumu zake zisizo za kiadilifu dhidi ya wanaharakati na wakosoaji wa utawala wa Aal-Khalifa, baada ya kutoa hukumu ya vifo na kifungo jela kwa wanaharakati kadhaa.

Gazeti la al-Wasat limeripoti kuwa, Hassan Isa, mmoja wa viongozi wa chama cha Kiislamu cha al-Wefaq amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela, kwa tuhuma bandia za 'kufadhili ugaidi'.

Mwanachuoni huyo ambaye pia alikuwa Mbunge wa chama cha al-Wefaq anatuhumiwa kuhusika katika hujuma iliyopelekea kuuawa maafisa wawili wa polisi na wengine kadhaa kujeruhiwa, madai ambayo amekuwa akiyakanusha vikali.

Namna utawala wa Manama unavyotumia mkono wa chuma dhidi ya waandamanaji wasio na silaha nchini Bahrain

Wakati huohuo, mahakama ya Bahrain imewahukumu adhabu ya kifo Mohammed Ibrahim al-Tawq na Mohammed Radi Abdullah, wanaharakati na wakosoaji wakubwa wa serikali wa Manama. Kadhalika wanaharakati wengine watano wamehukumiwa adhabu ya kifo, ambapo wanne kati yao wamepokonywa uraia.

Haya yanajiri wiki mbili baada ya utawala wa wa ukoo wa Aal-Khalifa kuakhirisha tena kutolewa hukumu dhidi ya Sheikh Isa Qassim, mwanazuoni mashuhuri wa Bahrain hadi Mei 7 mwaka huu. 

Utawala wa kiukoo wa Bahrain unamtuhumu Sheikh Qassim kwamba amekuwa akieneza chuki za kimadhehebu miongoni mwa watu wa  nchi hiyo, kuchochea machafuko na kuhatarisha usalama wa taifa.

Ikumbukwe kuwa nchi kadhaa za Kiarabu hususan Saudi Arabia zimetuma wanajeshi wao nchini Bahrain kwa ajili ya kuwakandamiza raia wanaoandamana kwa amani kupigania haki zao za kimsingi kabisa kama vile haki ya kujichagulia wenyewe viongozi wao.