Jeshi la Syria lakanusha kuhusika na utumiaji silaha za kemikali
(last modified Tue, 04 Apr 2017 16:11:11 GMT )
Apr 04, 2017 16:11 UTC
  • Jeshi la Syria lakanusha kuhusika na utumiaji silaha za kemikali

Jeshi la Syria limekadhibisha madai ya wapinzani kwamba limehusika na shambulio la silaha za kemikali katika mji wa Khan Sheikhoun, mkoani Idlib.

Kanali ya televisheni ya Sky News imenukuu duru moja ya jeshi la Syria ikitangaza kuwa jeshi la nchi hiyo halijawahi na wala halitotumia katu silaha za kemikali katika mashambulio yake.

Duru zenye mfungamano na magaidi na wapinzani wa Syria mapema leo zilidai kuwa ndege kadhaa za kivita zimeshambulia kwa makombora yenye gesi ya sumu yenye athari sawa na gesi ya sumu ya sarin mji wa Khan Sheikhoun katika mkoa wa Idlib kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Magaidi na wapinzani wamedai kuwa ndege hizo zilizofanya shambulio hilo ni za jeshi la Syria au Russia.

Magaidi hao aidha wamedai kwambaa watu wasiopungau 60 wameuawa na wengine 200 wamejeruhiwa katika hujuma hiyo.

Raia wa Syria akipatiwa huduma za tiba kufuatia hujuma ya silaha za kemikali 

Wakati huohuo baadhi ya vyombo vya habari vya eneo vimetangaza kuwa tukio la Idlib limesababishwa na mripuko wa ghala la mabomu ya kemikali inayomilikiwa na magaidi.

Mkoa wa Idlib hivi sasa ni ngome kuu ya makundi ya kigaidi na wapinzani wanaobeba silaha wanaoipinga serikali ya Syria, ambao walikimbilia katika mkoa huo kufuatia kukombolewa miji kadhaa ukiwemo wa Halab (Aleppo).../ 

Tags