Apr 25, 2017 04:49 UTC
  • Damascus yajibu propaganda chafu za Washington kuhusu silaha za kemikali

Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Syria amekadhibisha propaganda chafu zinazoenezwa na vyombo vya habari vya Kimarekani na kusisitiza tena kwamba Syria haina aina yoyote ya silaha za kemikali.

Faisal al Miqdad ameashiria habari za uongo zinazoenezwa na vyombo vya habari vya Marekani na washirika wake kwa ajili ya kuhalalisha shambulizi lililofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya kituo cha anga cha Shyrat huko magharibi mwa Syria, na kusema nchi hiyo haina silaha ya aina yoyote ya kemikali.

Naibu Waziri wa Mashauri ya kigeni wa Syria ameashiria pia majukumu yake ya kusimamia operesheni ya kuangamiza silaha zote za kemikali za nchi hiyo na kusema kuwa: Damascus ilizikabidhi nchi za Maghaibi nyaraka zote zinazuhusiana na kadhia hiyo. 

Faisal al Miqdad

Tarehe 7 mwezi huu wa Aprili Marekani ilishambulia kwa makombora kituo cha jeshi la anga la Syria huko Shayrat mkoani Idlib na kuua raia 9. Shambulizi hilo ambalo lilifanyika dhidi ya nchi inayojitawala bila ya idhini ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilifanyika kwa kisingizio kwamba serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali dhidi ya eneo la Khan Sheykhoun, suala ambalo linakadhibishwa na serikali ya Damascus.  

Tags