May 01, 2017 07:32 UTC
  • Jinai za ukoo wa Kifalme Bahrain zazidi kulaaniwa

Makundi ya haki za binadamu katika kona mbalimbali za dunia yamelaani jinai za ukoo wa Aal Khalifa dhidi ya wafungwa nchini Bahrain na kuutaka utawala huo kandamizi kuacha kuwanyanyasa wafungwa.

Kwa mujibu wa Press TV, makundi 10 ya haki za binadamu likiwemo la Human Rights Watch jana yalitoa taarifa na huku yakilaani unyanyasaji, mateso na ukandamizaji wanaofanyiwa wafungwa na maafisa wa ukoo wa Aal Khalifa, yameutaka ukoo huo uache mara moja kuwanyanyasa raia.

Makundi hayo aidha yamehimiza kufanyika uchunguzi wa kina kuhusu uvunjaji wa haki za binadamu unaofanyika kwenye jela za Bahrain na kuwataka watawala wa nchi hiyio kuheshimu sheria za kimataifa na kuruhusu wafungwa kuonana na familia zao na kupata huduma za afya.

Maandamano ya amani ya wananchi wa Bahrain

 

Wakati huo huo Joe Stork, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Human Rights Watch kuhusu Mashariki ya Kati amesema kuwa, hali ya haki za binadamu katika jela za Bahrain ni ya kusikitisha sana. Amesema, ukandamizaji wanaofanyiwa wafungwa nchini Bahrain ni mkubwa kiasi kwamba unawalazimisha watafute kila njia za kutoroka jela na kukwepa mateso hayo.

Wimbi la mapinduzi ya wananchi liliikumbwa Bahrain tarehe 14 Februari 2011. Wananchi wa nchi hiyo wanapigania haki zao za kimsingi kabisa, kama vile haki ya kujichagulia wenyewe viongozi wao. Baadhi ya nchi za Kiarabu hususan Saudi Arabia zimetuma wanajeshi wao nchini humo ili kukandamiza maandamano ya amani ya wananchi hao.

Tags