May 26, 2017 13:15 UTC
  • Ukandamizaji usiokoma wa Aal Khalifa dhidi ya wananchi wa Bahrain

Katika hali ambayo Wabahrain wamekuwa wakifanya maandamano ya kulalamikia hukumu ya kifungo cha jela iliyotolewa hivi karibuni dhidi ya Sheikh Issa Qassim, hatua ya watawala wa nchi hiyo ya kutoa hukumu nyingine ya kidhalimu ya kubadili kifungo cha miaka 2 jela kuwa cha maisha kwa watuhumiwa wengine 16 na vilevile kupokonywa uraia Wabahrain wengiene wanane ni ishara tosha kwamba ukandamizaji wa watawala hao dhidi ya raia wa nchi hiyo bado unaendelea.

Mahamaka ya Aal Khalifa siku ya Alhamisi ilitoa hukumu za kidhalimu dhidi ya raia 24 wa nchi hiyo kwa tuhuma zisizo na msingi kwamba walihusika na kubuni makundi ya uharibifu na uhalifu nchini humo. Ni muhimu kutaja hapa nukta mbili kuhusiana na hukumu hizo. Ya kwanza ni kuwa kwa kutoa hukumu hizo za kidhalimu utawala wa mabavu wa Aal Khalifa unakususia kuzua hofu na woga miongoni mwa raia wa nchi hiyo ili kuwazuia kuendelea na malalamiko na maandamano ya kupigania haki zao za msingi. Malalamiko na maandamano ya Wabaharain yameongezeka katika siku za hivi karibuni tokea mahakama ya Bahrain ilipotoa hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja dhidi ya Sheikh Issa Qassim na vilevile kupokonywa mali zake zote.

Sheikh Isa Qassim wa Bahrain

Licha ya kuwaua raia watano katika maandamano hayo utawala wa Bahrain umejeruhi makumi ya wengine na kutia nguvuni mamia ya wengine. Utawala huohuo umekuwa ukitumia vibaya vyombo vya mahakama kwa ajili ya kutekeleza aina nyingine ya dhulma dhidi ya raia wa nchi hiyo, kwa kuvilazimisha vitoe hukumu za vifungo vya muda mrefu, kuvua uraia na kuwanyima watuhumiwa haki zao za kiraia ili kuthibitisha kwamba njia pekee ya kuzima malalamiko yao ni kutumia mabavu na ukandamizaji dhidi yao. Nukta ya pili ni kwamba utawala wa Bahrain unataka kutoa ujumbe huu kwamba licha ya kupita miaka 6 ya malalamiko ya wananchi lakini bado vyombo vya dola vinauunga mkono utawala huo. Ni kwa msingi huo ndio maana ukawa unatumia vyombo vya usalama kujaribu kuzima maandamano ya wananchi na pia vyombo vya mahakama kutuoa hukumu zinazoupendelea utawala huo kwa madhara ya raia. Utawala wa Manama unajaribu kutoa ujumbe huo katika hali ambayo sehemu kubwa ya askari usalama wa nchi hiyo inaundwa na askari vibaraka wa kigeni ambao wanalipwa kwa ajili ya kuwakandamiza raia wa Bahrain, jambo ambalo lenyewe linachochea hisia kali za Wabahrain na hata kuwafanya wazidishe azma yao ya kuendeleza malalamiko na harakati za kupigania haki zao.

Ukandamiza unaofanywa na askari wa Bahrain dhidi ya raia wa nchi hiyo

Hii ni kwa sababu kama utawala wa Aal Khalifa usingewatumia mamluki hao wa kigeni kuwakandamiza Wabahrain bila shaka kiwango cha machafuko na ukandamizaji dhidi ya raia kingepungua kutokana na hisia ya utaifa katika pande mbili, na hivyo kuandaa uwanja wa kufanyika mazungumzo kati ya serikali na wapinzani. Kutumiwa askari wa kigeni ambao kimsingi wanatokja nchi masikini kwa ajili ya kuwakandamiza Wabahrain kumepelekea baadhi ya taasisi za kimataifa kulalamikia suala hilo. Kuhusu jambo hilo hivi karibuni Shirika la Msamaha Duniani, Amnesty International, lililalamikia vikali hatua ya mahakama za Bahrain kutoa hukumu za kidhalimu dhidi ya watuhumiwa ambao wamelazimishwa kukiri makosa ambayo hawakuhusika nayo tena katika mazingira magumu ya mateso, kupigwa, kujeruhiwa na kufanyiwa vitendo visivyofaa.

Tags