Jun 28, 2017 07:18 UTC
  • Hizbullah: Mpango wa matakfiri Mashariki ya Kati unasambaratika

Harakati ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa, hali ya kisiasa inayotawala hivi sasa katika eneo la Mashariki ya Kati ni kwa manufaa ya mhimili wa muqawama na kwamba, mpango wa matakfiri umo katika katika hali ya kusambaratika.

Hayo yameelezwa na Sheikh Ali Damush, Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon ambaye amebainisha kuwa, lugha za vitisho za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Hizbullah zimepungua. 

Ameongeza kuwa, hali imebadilika katika matamshi ya viongozi wa kisiasa na kijeshi wa Israel kiasi kwamba, wanasema bayana kuwa, hawana nia ya kuingia katika vita na Hizbullah ya Lebanon.

Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon amesema wazi kuwa, Israel inaogopa kupigana vita na Lebanon kwani inafahamu vyema nguvu na uwezo wa wapiganaji wa Hizbullah.

Wapiganaji wa Hizbullah

Aidha Sheikh Ali Damush amesisitiza kuwa, viongozi wa Israel wanafahamu vyema kwamba, endapo Tel Aviv itaingia katika vita na Hizbullah itapata hasara kubwa. 

Viongozi wa utawala ghasibu wa Israel wakiwemo wa kisiasa na kijeshi wamekuwa wakikiri mara kwa mara juu ya uwezo mkubwa wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon.

Hivi karibuni Moshe Arens, waziri wa zamani wa vita wa utawala haramu wa  Israel alisema kuwa, makombora ya harakati ya muqawama wa Kiislamu wa Hizbullah ya Lebanon, ndio hatari kubwa zaidi inayoukabili utawala huo ghasibu.

 

 

Tags