Israel: Wakati wa kuwekwa wazi mahusiano yetu na Saudia, umewadia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i32234-israel_wakati_wa_kuwekwa_wazi_mahusiano_yetu_na_saudia_umewadia
Gazeti la utawala haramu wa Israel limezungumzia mahusiano yaliyopo baina ya Israel na Saudi Arabia na kuandika kuwa sasa umewadia wakati wa kutangazwa wazi mahusiano ya pande mbili hizo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 25, 2017 03:47 UTC
  • Israel: Wakati wa kuwekwa wazi mahusiano yetu na Saudia, umewadia

Gazeti la utawala haramu wa Israel limezungumzia mahusiano yaliyopo baina ya Israel na Saudi Arabia na kuandika kuwa sasa umewadia wakati wa kutangazwa wazi mahusiano ya pande mbili hizo.

Gazeti la Maariv la Israel sambamba na kuweka wazi uungaji mkono wa siri wa Tel Aviv kwa Saudia, limekosoa pia siasa za baraza la mawaziri la Israel za kuendelea kuficha mahusiano yake na Riyadh na kuongeza kuwa, kwa kuzingatia kwmba Saudia inaihitajia sana Israel, sasa umefika wakati wa kutangazwa waziwazi mahusiano hayo. Kadhalika Maariv limeitaka serikali ya utawala wa Kizayuni kuacha kukanusha kuwepo mikutano ya siri na Wasaudi na badala yake itumikie maslahi ya Israel.

Kabla ya hapo  Yisrael Katz, Waziri wa Intelejensia na Ujasusi wa Israel alitoa pendekezo kwa Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud akimtaka kumwalika Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala huo kufanya safari nchini Saudia.

Yisrael Katz, Waziri wa Intelejensia na Ujasusi wa Israel

Kwa mujibu wa Katz, Tel Aviv inaweza kushirikiana na Saudia na hata nchi za eneo la Ghuba ya Uajemi katika masuala ya intelejensia na ujasusi mkabala ya kuboresha mahusiano wa Riyadh na utawala huo.

Ushirikiano wa Saudia na Israel umekuwa ukidhihiri zaidi hususan baada ya Riyadh kutekeleza siasa za kukabiliana na harakati za muqawama katika eneo la Masharuiki ya Kati na kadhalika uungaji mkono wa Aal Saud kwa magaidi.