Ibrahim al-Jaafari: Msimamo wa Iraq kuhusu kadhia ya Palestina haujabadilika
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i33534-ibrahim_al_jaafari_msimamo_wa_iraq_kuhusu_kadhia_ya_palestina_haujabadilika
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iraq amesema kuwa, nchi yake ingali inaunga mkono kadhia ya Palestina na malengo matukufu ya taifa hilo madhulumu na kwamba, msimamo wa Baghdad kuhusiana na kadhia hiyo haujabadilika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 23, 2017 09:35 UTC
  • Ibrahim al-Jaafari: Msimamo wa Iraq kuhusu kadhia ya Palestina haujabadilika

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iraq amesema kuwa, nchi yake ingali inaunga mkono kadhia ya Palestina na malengo matukufu ya taifa hilo madhulumu na kwamba, msimamo wa Baghdad kuhusiana na kadhia hiyo haujabadilika.

Dakta Ibrahim al-Jaafari amesema hayo alasiri ya leo mjini Baghdad katika mkutano wake na waandishi wa habari akiwa pamoja na Riyadh al-Maliki, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Palestina na kusisitiza kwamba, Iraq itaendelea kuiunga mkono kadhia ya Palestina.

Dakta Ibrahim al-Jaafari amebainisha kuwa, tangu mgogoro wa Palestina ulipoanza, Marajii Taqlidi wa Iraq wamekuwa wakisisitiza juu ya udharura wa kusaidia juhudi za kusukuma mbele malengo matukufu ya Palestina.

Wanajeshi wa Israel wakiuvamia msikiti wa al-Aqswa

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iraq ameelezea pia azma ya serikali ya Baghdad ya kustafidi na wataalamu wa Kipalestina walioko katika maeneo mbalimbali ulimwenguni kwa ajili ya kuikarabati Iraq.

Kwa upande wake, Riyadh al-Maliki, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Palestina ameiisifu na kuipongeza Iraq kutokana na msimamo wake wa kuunga mkonono kadhia ya Palestina na malengo yake matukufu na kuongeza kuwa, kwa muda mrefu Baghdad imekuwa ikiunga mkono suala la Palestina na mapambano yake dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.

Ameongeza kuwa, katika duru za kieneo la kimataifa, Iraq imekuwa ni mkumbushaji wa kadhia ya Palestina na haighafiliki na msimamo wake na kwamba, jambo hilo lina umuhimu mno kwa wananchi madhulumu wa Palestina.