Bashar al Assad: Maadui wataendelea kupata kipigo
(last modified Mon, 28 Aug 2017 04:00:08 GMT )
Aug 28, 2017 04:00 UTC
  • Bashar al Assad: Maadui wataendelea kupata kipigo

Rais wa Syria amesema kuwa maadui wataendelea kupata kipigo madhali irada ya muqawama inaendelea kuwepo katika nyoyo na nafsi za vijana wa Syria.

Rais Bashar al Assad wa Syria amesema kuwa lengo la maadui tangu awali huko Syria lilikuwa ni kuzima shaari ya muqawama, hata hivyo wenyewe ndio wamefeli katika njia hiyo. Rais wa Syria amesema hayo jana Jumapili alipokutana na kufanya mazungumzo na washiriki wa mkutano wa pili wa "Vijana wa Kiarabu Wanamuqawama." 

Akiwahutubu vijana wa Syria, Rais Bashar al Assad amebainisha kuwa jukumu la vijana mkabala na changamoto zilizopo sasa katika eneo ni kujenga mustakbali wa Syria. 

Rais wa Syria ameongeza kusema kuwa maadui tangu kitambo nyuma walipanga njama ili kuzima harakati ya muqawama, hata hivyo hii leo vikosi vya wanamuqawama vimezishinda njama hizo za maadui.