Israel yavunja zaidi ya misikiti na makanisa 50 Palestina
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i34807-israel_yavunja_zaidi_ya_misikiti_na_makanisa_50_palestina
Walowezi wa Kizayuni wamevunja misikiti na makanisa yasiyopungua 53 katika kipindi cha miaka minane (8) iliyopita katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 25, 2017 00:40 UTC
  • Israel yavunja zaidi ya misikiti na makanisa 50 Palestina

Walowezi wa Kizayuni wamevunja misikiti na makanisa yasiyopungua 53 katika kipindi cha miaka minane (8) iliyopita katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Kituo cha upashaji habari cha Palestina jana (Jumapili) kilitangaza kwamba, kwa mujjibu wa ripoti za karibuni kabisa, tangu mwaka 2009 hadi hivi sasa, walowezi wa Kizayuni na wanajeshi wa Israel wamefanya uhalifu mkubwa katika maeneo matakatifu ya Waislamu na Wakristo huko Palestina.

Kasisi wa Kanisa la Multiplication kaskazini mwa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu akikagua kanisa lake baada ya kuchomwa moto na Wazayuni

 

Wataalamu wa mambo wanasema kuwa, katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, utawala wa Kizayuni wa Israel umetangaza vita rasmi vya kidini dhidi ya Wapalestina bila ya kujali itikadi na dini zao. Ni jambo lililo wadhiha kwa watu wote, kwamba utawala wa Kizayuni hauheshimu mafundisho ya dini yoyote ile, hususan pale yanapokwenda kinyume na fikra za Kizayuni.

Jana Jumapili pia, Wazayuni walishambulia vitongoji kadhaa vya Wapalestina vikiwemo vya al Khalil na Qalqilya na kuwateka nyara Wapalestina wasiopungua 14.

Kanisa la Miracle la Wakristo wa Palestina baada ya kuchomwa moto na kuvunjwa na walowezi wa Kizayuni

 

Kila siku wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wanavamia maeneo ya Wapalestina na kuwateka nyara vijana wa taifa hilo madlumu bila ya makosa yoyote.

Takwimu za taasisi mbalimbali za Palestina zinasema kuwa, hivi sasa kuna Wapalestina 6400 katika jela za kuogofya za Wazayuni huku 62 kati ya Wapalestina hao wakiwa ni wanawake na 300 wengine ni watoto wadogo.