Idadi ya wanajeshi wa Israel wenye matatizo ya kisaikolojia yaongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i3667-idadi_ya_wanajeshi_wa_israel_wenye_matatizo_ya_kisaikolojia_yaongezeka
Duru za Kizayuni zimeripoti kuwa maradhi ya kisaikolojia yanazidi kuenea miongoni mwa wanajeshi wa utawala huo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 23, 2016 21:29 UTC
  • Idadi ya wanajeshi wa Israel wenye matatizo ya kisaikolojia yaongezeka

Duru za Kizayuni zimeripoti kuwa maradhi ya kisaikolojia yanazidi kuenea miongoni mwa wanajeshi wa utawala huo.

Gadi Lubin, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari wa Israel jana alieleza kuwa maelfu ya wanajeshi wa utawala huo wanasumbuliwa na maradhi ya kiakili na katika hao waliopatwa na maradhi hayo, wapo majenerali, maafisa wa jeshi na marubani kadhaa.

Wakati huo huo maafisa wa jeshi wai utawala wa Kizayuni wamekiri kuwa wanajeshi kadhaa wa utawala huo wametoroka kwenye kambi zao. Wanajeshi hao wametoroka makambini kufuatia kupamba moto Intifadha ya Quds tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi wa Israel hawawezi kukabiliana na oparesheni za kimuqawama za Wapalestina ikiwemo ya kutekeleza mashambulizi kwa kutumia silaha baridi.

Wapalestina wamekwishawaangamiza Wazayuni 33 na kuwajeruhi wengine wengi tangu kuanza Intifadha ya Quds mwanzoni mwa mwezi Oktoba mwaka jana hadi hivi sasa; hiyo ikiwa ni katika kujibu jinai za utawala wa KIzayuni dhidi ya raia wa Wapalestina.