Syria yaahidi kujibu jinai zote za Israel nchini humo
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria ameuonya utawala wa Kizayuni na kuuhakikishia kuwa Damascus itajibu mashambulizi yote yanayofanywa na Israel katika ardhi ya Syria.
Feisal al Miqdad amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na televisheni ya al Alam na kuongeza kuwa, uchokozi wa Israel wa kufanya mashambulizi ndani ya ardhi ya Syria na vile vile uungaji mkono wa Marekani kwa genge jipya la kigaidi linalojulikana kwa jina la "Vikosi vya Demokrasia nchini Syria" (قسد QSD) hautaachwa vivi hivi kwani mtu yeyote anayechukua silaha kupigana na serikali halali ya Syria huyo ni gaidi.
Al Miqdad ameongeza kuwa, genge hilo jipya la kigaidi linafanya fitna katika eneo la kaskazini mashariki mwa Syria likiwa katika kutumikia ubeberu wa Marekani dhidi ya taifa na serikali ya Syria, hivyo Damascus inatoa onyo kwamba kama genge hilo litaendelea na fitna zake basi mwisho wake utawakuwa sawa na ule wa magenge ya kigaidi ya Daesh (ISIS), Jabhatun Nusra na magenge mengine ya watenda jinai.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria aidha amesema kuwa, kwa msaada wa marafiki zake, nchi yake imeweza kusimama imara kukabiliana na uvamizi wa maadui na kuongeza kuwa, Syria na waitifaki wake wamefanikiwa kuliangamiza kikamilfu genge la kigaidi la Daesh nchini humo.
Amesema, labda tunaweza kusema kuwa, Syria ndiyo nchi pekee ya Kiarabu ambayo licha ya kukumbwa na migogoro mbalimbali, bado imesimama imara kuliuga mkono taifa linalodhulumiwa la Palestina.