Hizbullah yautahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i39701-hizbullah_yautahadharisha_utawala_wa_kizayuni_wa_israel
Harakati ya Hizbullah ya lebanon imeutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kupitia kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilichopo kusini mwa Lebanon (UNIFIL) kuhusu suala la kujenga ukuta wa kibaguzi katika mipaka na Lebanon.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 31, 2018 03:22 UTC
  • Hizbullah yautahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel

Harakati ya Hizbullah ya lebanon imeutahadharisha utawala wa Kizayuni wa Israel kupitia kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kilichopo kusini mwa Lebanon (UNIFIL) kuhusu suala la kujenga ukuta wa kibaguzi katika mipaka na Lebanon.

Kanali ya pili ya televisheni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imetangaza kuwa, harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetishia kuwa itawafyatulia risasi wanajeshi wa Israel iwapo utawala wa Kizayuni hautasimamisha ujenzi wa ukuta wa kibaguzi katika mipaka na Lebanon. 

Tovuti ya Israel 24 imeinukuu kanali ya pili ya televisheni ya utawala huo na kuandika kuwa, askari jeshi wa kikosi cha UNIFIL wamewatumia ujumbe mabalozi wa Uingereza na Marekani wakihofia kuibuka mivutano na kutaka ujumbe huo ufikishwe kwa Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Ukuta huo mpya eti wa usalama unaofanana na ule uliojengwa na Israel katika mpaka wa Misri, utajengwa katika mpaka na Lebanon huku ukiwa na kilomita 30 na urefu wa mita sita. Ujenzi wa ukuta huo utagharimu dola milioni 28. 

Uzio wa eneo kutakapojengwa ukuta wa kibaguzi wa Israel huko kusini mwa Lebanon 

Kabla ya hapo, Baraza Kuu la Ulinzi la Lebanon lilisisitiza kwamba azma ya utawala wa Kizayuni ya kujenga ukuta katika maeneo ya mipaka na Lebanon ni ukiukaji wa azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kwamba litachukua hatua zote za lazima kuzuia ujenzi wa ukuta huo wa kibaguzi.

Azimio nambari 1701 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilipasishwa baada ya kumalizika vita vya siku 33 vilivyoanzishwa na Israel dhidi ya Lebanon, linautaka utawala wa Kizayuni ujiepushe na hatua za kiuhasa dhidi ya Lebanon. Hata hivyo utawala huo ghasibu umekuwa ukipuuza azimio hilo na kukiuka anga, mipaka ya nchi kavu na baharini ya nchi hiyo.