Jun 28, 2018 02:36 UTC
  • Kutowezekana kupatiwa ufumbuzi mgogoro wa Yemen kwa mtutu wa bunduki

Baraza la Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Ulaya limesisitiza kuwa, mgogoro wa Yemen hauwezi kupatiwa ufumbuzi kwa njia za kijeshi na kwamba, ufumbuzi pekee ni kupatikana amani ya kudumu kupitia njia ya mazungumzo.

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Ulaya wamesisitiza hilo mbele ya Martin Griffiths, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen. Mawaziri hao kwa mara nyingine tena wamesisitiza kwamba, kadhia ya Yemen haiwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi. Umoja wa Ulaya ambao umekuwa ukishirikiana na pande zinazozozana nchini Yemen, umeeleza utayarifu wake wa kuongeza zaidi nafasi yake huko Yemen husuasan katika suala zima la utumaji misaada ya kibianadamu.

Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Ulaya aisha wamesisitiza kwamba, amani ya kudumu nchini Yemen inawezekana kupatiana tu kupitia mazungumzo ambayo yatazishirikisha pande na mirengo yote ya nchi hiyo.

Martin Griffiths, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen

Licha ya kuwa Umoja wa Ulaya unasisitiza kutumiwa njia ya kisiasa kwa ajili ya kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Yemen, lakini baadhi ya nchi za Ulaya ni wadhamini wakuu wa silaha za utawala wa Aal Saud wa Saudi Arabia. Mikataba ya silaha baina ya nchi za Ulaya na utawala wa Riyadh ni jambo ambalo katika miezi ya hivi karibuni limekosolewa mara chungu nzima na fikra za waliowengi barani Ulaya na jamii ya kimataifa. Licha ya madai ya Umoja wa Ulaya na marufuku kwa wanachama wake ya kuiuzia silaha Saudi Arabia lakini ukweli wa mambo ni kuwa kivitendo umoja huo hauna imani na hilo.

Nchi za Ulaya kama Ujerumani na Uingereza zimetiliana saini na Saudia mikataba ya mabilioni ya dola. Hatua ya nchi hizo ya kutanguliza mbele maslahi yao ya kiuchumi kupitia biashara ya silaha  ndio iliyopelekea hali ya kibinadamu nchini Yemen izidi kuwa mbaya siku baada ya siku. Kwa maneno mengine ni kuwa, madola hayo yameamua kutanguliza mbele maslahi yao ya kiouchumi na kuweka kando utu na ubinadamu.

Kampeni ya kupinga kuuziwa silaha Saudi Arabia

Nchi kama Uingereza ikiwa na lengo la kuendelea kupata pato nono la mauzo ya silaha iikiziunga mkono kisiasa na kijeshi Saudia na Imarati ambazo zinanunua silaha za dola hilo la Kimagharibi. Aidha uchunguzi uliofanywa na mashirika ya kutetea haki za binadamu unaonyesha kwamba, mabomu yaliyotumiwa na muungano unaoongozwa na Saudi Arabia kaskazini magharibi mwa Yemen yalitengenezwa nchini Italia.

Mashirika ya kutengeneza silaha na madola ya Ulaya yamekuwa yakipata faida kubwa mno kupitia vita kutokana na kuuza silaha. Hatua hiyo kabla ya kuwa ni ukiukaji wa sheria za kimataifa inakinzana na utu na misingi ya kimaadili.

Hii ni kutokana na kuwa, kuiuzia silaha nchi kama Saudia ni kusaidia kutenda jinai. Bénédicte Jeannero, Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Huma Rights Watch nchini Ufaransa anasema kuwa, Saudia inaongoza muungano wa kijeshi ambao hadi sasa umeua maelfu ya raia nchini Yemen, mauaji ambayo yanapaswa kuhesabiwa kuwa ni9 jinai za kivita.

Hujuma ya kijeshi ya Saudi Arabia nchini Yemen

Ikiwa Ulaya itaendelea kuiuzia silaha Saudi Arabia itakuwa mshirika wa jinai za kivita na ukiukaji wa sheria za kiimataifa. Madola yanayoudhaminia silaha utawala wa Aal Saud licha ya matakwa ya mara kwa mara kieneo na kimataifa yanayowataka kusitisha kuiuzia silaha Saudia, lakini hadi sasa hayajachukua hatua yoyote ile ya maana.

Umoja wa Mataifa pamoja na wajumbe wake maalumu, mara kadhaa wamesisitiza kwamba, mgogoro wa Yemen hauwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi bali njia pekee ni ufumbuzi wa kisiasa na kidiplomasia. Licha ya msisitizo huo wa kila mara, lakini asasi, jumuiya za kimataifa na baadhi ya nchi za Ulaya  zikiwa na lengo la kunufaika kiuchumi zimeendelea kuzipatia silaha pande zinazopigana nchini Yemen na kivitendo kuunga mkono ufumbuzi wa kijeshi katika kadhia ya Yemen.

Tags