Wazayuni wawapiga na kuwatukana wanawake wa Palestina
(last modified Tue, 21 Aug 2018 07:36:53 GMT )
Aug 21, 2018 07:36 UTC
  • Wazayuni wawapiga na kuwatukana wanawake wa Palestina

Wanajeshi katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wamewapiga na kuwashambulia kwa maneno wanawake kadhaa wa Kipalestina.

Kituo cha Upashaji Habari cha Palestina kimeripoti kuwa, wanajeshi wa Israel jana waliwavamia wanawake kadhaa wa Kipalestina katika masoko ya eneo la kale la mji mtakatifu wa Quds na katika barabara ya Salahud Din na kuwapiga, kuwashambulia kwa maneno na kupondaponda mazao yao ya kilimo.

Si hayo tu, lakini pia wanajeshi hao wamewaondoa kikatili wanawake wa Palestina waliokuwa wakitafuta riziki zao kupitia kuuza bidhaa katika Soko la Quds.

Ukandamizaji wa wanajeshi katili wa Israel dhidi ya Wapalestina

 

Lengo la utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuuyahudisha mji wa Baytul Muqaddas na ndio mara kwa mara inafanya jinai kama hizo dhidi ya Wapalestina ili kuwalazmisha wahame. Wakulima na wafanya biashara ni miongoni mwa wahanga wakuu wa jinai hizo za Israel.

Wakati huo huo wanajeshi wa Israel wamevivamia vitongoji vya al Khalil, Ramallah, Nablosi, Qilqilya na Quds na kuwateka nyara Wapalestina 11 na kuwapeleka kusikojulikana.

Suala la kuvamiwa nyumba za Wapalesitna katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na katika mji wa Quds ni jambo la kila siku linalofanywa na wanajeshi makatili wa Israel kwa visingizio tofauti.

Tags