Aug 25, 2018 13:46 UTC
  • Saudia inatumia vibaya fedha zinazotokana na ibada ya Hija

Kamati ya Kimataifa ya Uangalizi wa Usimamizi wa Saudia juu ya Ibada ya Hija, imesema kuwa, utawala wa Aal-Saud unatumia vibaya pato linalotokana na ibada ya Hija.

Taarifa iliyotolewa na kamati hiyo imesema kuwa, watawala wa Saudi Arabia wanawalazimisha maelfu ya mahujaji kulipa kodi kubwa kwa ajili ya kutekeleza ibada hiyo. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, utawala na viongozi wa Aal-Saud wanalipa tu umuhimu suala la pato linalotoka kwa mahujaji, kama ambavyo hawayapi umuhimu wowote mahitaji ya mahujaji wala kulinda turathi za Kiislamu. Kamati ya Kimataifa ya Uangalizi wa Usimamizi wa Saudia juu ya Ibada ya Hija sambamba na kufichua utumiaji mbaya wa  utawala huo ibada ya Hija kwa maslahi ya kiuchumi ya utawala huo, kwa mara nyingine imetaka ushiriki wa asasi na serikali za Kiislamu juu ya usimamizi wa ibada ya Hija na maeneo matukufu ya Haram Mbili.

Gharama za kupenda vita zinawafanya viongozi wa Saudia kuwatoza kodi kubwa mahujaji

Kwa kuzingatia kupanda ghama za kijeshi za Saudia katika vita vyake nchini Yemen, hivyo ibada ya Hija imegeuka na kuwa ingizo la pato muhimu kwa ajili ya nchi hiyo. Katika uwanja huo hivi karibuni pia Omar Marwan mwakilishi wa serikali ya Misri katika masuala ya Bunge na kiongozi wa msafara wa Hija wa Misri, alinukuliwa akisema kuwa, Saudi Arabia inafidia nakisi ya bajeti yake ya mwaka kwa kuzidisha gharama za ibada ya Hija, suala ambalo limewakasirisha mno mahujaji kutoka nchi mbalimbali hususan mahujaji kutoka Misri.

Tags