UN: Wakimbizi 30 elfu wanahitajia misaada ya haraka, mashariki mwa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i48473-un_wakimbizi_30_elfu_wanahitajia_misaada_ya_haraka_mashariki_mwa_syria
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, kuna wakimbizi 30 elfu waliokimbia makazi yao mashariki mwa Syria kutokana na mashambulizi ya miezi mitatu iliyopita dhidi ya maeneo ya magaidi wa Daesh (ISIS) mkoani Deir ez-Zor.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 29, 2018 21:55 UTC
  • UN: Wakimbizi 30 elfu wanahitajia misaada ya haraka, mashariki mwa Syria

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, kuna wakimbizi 30 elfu waliokimbia makazi yao mashariki mwa Syria kutokana na mashambulizi ya miezi mitatu iliyopita dhidi ya maeneo ya magaidi wa Daesh (ISIS) mkoani Deir ez-Zor.

Stéphane Dujarric, msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari mjini New York Marekani kuwa, kwa mujibu wa ripoti za maafisa wa Umoja wa Mataifa na taasisi za misaada ya kibinadamu, mshambulizi ya kijeshi dhidi ya genge la kigaidi la Daesh katika mkoa wa Deir ez-Zor yaliyoanza mwezi Juni 2018 yamepelekea watu 30 elfu kuyakimbia makazi yao.

Amesema hali ya wakimbizi hao ni mambo sana na hawana suhula zozote za lazima zikiwemo za afya huku baadhi yao wakiwa wanahitajia huduma za haraka za tiba.

Uharibifu mkubwa uliofanywa na mashambulizi ya Marekani huko Deir ez-Zor, Syria

 

Tangu mwaka 2014, Marekani na kundi lake wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Syria kwa madai ya kupambana na magaidi ya Daesh (ISIS) licha ya kwamba mashambulizi hayo hayana baraka zozote za Umoja wa Mataifa na wala idhini ya serikali ya Syria. Marekani ina wanajeshi wake ndani ya ardhi ya Syria kinyume kabisa na sheria za kimataifa na bila ya kupewa ruhusa na serikali ya nchi hiyo.

Mara kwa mara Marekani imekuwa ikitoa ripoti ya kukiri kwamba inaua raia wengi katika nchi za Iraq na Syria kwenye mashambulizi yake ya anga ambayo inadai yanalenga magaidi wa Daesh.