Saudia na Imarati zinaongoza kwa kununua vifaa vya kijasusi vya Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i48935-saudia_na_imarati_zinaongoza_kwa_kununua_vifaa_vya_kijasusi_vya_israel
Gazeti la Kizayuni la Haaretz limefichua kuwa, Bahrain, Imarati (UAE) na Saudi Arabia zina mikataba mikubwa sana ya kununua vifaa vya kijasusi kutoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 21, 2018 02:37 UTC
  • Saudia na Imarati zinaongoza kwa kununua vifaa vya kijasusi vya Israel

Gazeti la Kizayuni la Haaretz limefichua kuwa, Bahrain, Imarati (UAE) na Saudi Arabia zina mikataba mikubwa sana ya kununua vifaa vya kijasusi kutoka kwa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Gazeti hilo la Kizayuni limeandika: Israel inashika nafasi ya kwanza kwa kutumia zana za kijasusi na za udukuzi wa mazungumzo ya simu.

Limesema, vifaa vya kijasusi vinawasaidia majasusi kuingia katika kurasa za Intaneti na b-pepe au simu za mkononi za watu na kupata taarifa zao za ndani.

 

Kwa upande wake, mtandao wa Kizayuni wa Wall umeripoti kuwa wizara ya usalama wa ndani ya Israel limeyaruhusu makampuni mawili ya utawala wa Kizayuni kuipa huduma zake Saudi Arabia.

Naye Yusi Malman, mmoja wa watu walio karibu na shirika la usalama wa ndani la Israel amefichua kuwa, kampuni ya AGT International ambayo inasimamiwa na mfanya biashara mmoja Mzayuni wa Kimarekani, imefunga mikataba ya mamilioni ya dola na serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) katika masuala ya usalama.

Gazeti la Yedioth Ahronoth nalo limefichua kuwa, kampuni moja ya Israel inayojihusisha na masuala ya kijasusi inatoa mafunzo maalumu ya kijasusi na kiintelijensia kwa wanajeshi wa Imarati hususan mbinu za kulinda sehemu za mafuta na maeneo nyeti ya kiusalama.